MAMBO YA KUOMBEA JUMANNE: 12 JANUARI 2021

WIKI MBILI ZA KUFUNGA NA KUOMBA: DPC
11-23 Januari 2021

MAMBO YA KUOMBEA JUMANNE: 12/1/2021

  1. Jinyenyekeze mbele za Mungu, safisha mikono yako na utakase moyo wako kwa kutubu dhambi zako na kumwomba Mungu akusamehe na abadilishe maisha yako. Yakobo 4: 7-8, 1Timotheo 2: 8, Zaburi 24: 4
  2. Omba kubadilishwa nia yako ili uweze kujua na kukubali mapenzi ya Mungu yaliyo makamilifu kwa ajili ya maisha yako. Warumi 12: 2, Ezekieli 36:26. Luka 5: 36-39
  3. Angusha kila ngome katika akili yako na kila kitu ambacho ni kinyume na neno la Mungu. Teka kila fikra ipate kumtii Kristo. Warumi 1:21, 2Wakorintho 10: 4-5
  4. Mshukuru Mungu na utangaze kwamba una nia ya Yesu Kristo ndani yako. Mshukuru Mungu kwa sababu utayaona mambo jinsi Mungu aonavyo .
    1Wakorintho 2:16. Mshukuru Mungu kwa sababu anafanya jambo jipya katika maisha yako na katika kanisa.
    Isaya 43: 18-19

Join the Discussion

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top