MAOMBI YA ALHAMISI 16/7/2020.

WIKI MOJA YA KUFUNGA NA KUOMBA DPC
13-18 JULAI 2020
MAOMBI YA ALHAMISI 16/7/2020.

Mathayo 6:12 Utusamehe makosa yetu, kama nasi tunavyowasamehe waliotukosea

  1. Kiri na utubu dhambi zako, (udhaifu wowote, kutokuamini, kutokusamehe, nk) na uwasemehe wale walikukosea. 1 Yohana 1:8-10. Waefeso 4:22-32. Omba damu ya Yesu ikutakase, na kisha uombe nguvu za Roho Mtakatifu zikubadilishe na kukusaidia kutembea katika pendo la Mungu.
    Waefeso 5:1-21, Wagalatia 5:22-23
  2. Simama mahali palipobomoka na utubu kwa ajili ya familia yako. Ayubu 1:5. Omba rehema na neema ya Mungu juu yao kwa kila dhambi waliyotenda. Ombea wote ambao hawajaokoka waokolewe na kumtumikia Mungu 1 Timotheo 2:3-5, Yoshua 24:14. Ng’oa kila pando asilolipanda Mungu kwenye familia yako na uombe baraka za Mungu juu ya familia yako. Mathayo 15:13, 2 Wakorintho 10:4-5.
  3. Ombea familia ya DPC kwamba kila mshirika na wote wanaokuja kuabudu hapa wabadilishwe, watembee katika hofu ya Mungu na kujitoa kumtumikia kwa mioyo yao yote. Wakolosai 1:10; 4:12, Marko 12:30-31.
  4. Omba na usimame mahali palipobomoka kwa ajili ya taifa la Tanzania kama Danieli alivyoomba na kutubu kwa ajili ya taifa la Israeli. Danieli 9:4-19. Ezekieli 22:30, 2 Nyakati 7:13-14. Kiri dhambi zilizotendeka ndani ya Taifa letu kadri Roho wa Mungu atakavyokuongoza, omba Mungu aturehemu. Omba utakatifu, haki na hofu ya Mungu kutawala katika taifa letu. Mithali 14:34.

Join the Discussion

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top