SIKU 21 ZA KUFUNGA NA KUOMBA – 20/01/2024 (Siku ya 13)
UINJILISTI NA UMISHENI (KUPANDA MAKANISA) , BARAKA ZA MUNGU KATIKA FAMILIA ZETU,
BARAKA ZA MUNGU KATIKA FAMILIA ZETU,
1. Omba Mungu azibariki kazi za mikono yako. Kumb 15:6, Kumb 28:8, Zab 21: 3 & 6
2. Omba Mungu aibariki familia yako. Isaya 54:13
3. Omba Mungu akutane na haja za moyo wako Zab 21: 2, Isaya 3:10
a. Ki-Elimu
b. Ki-Uchumi
c. Ki-familia
4. Omba Mungu akupe KIBALI machoni pake na kwa watu wake. 1Samweli 2:26
UINJILISTI NA UMISHENI (KUPANDA MAKANISA)
1. Omba Mungu akutumie kuipeleka Injili ya Bwana wetu Yesu Kristo kwa wengine. Mathayo 28:18-20, 10:15b, Isaiah 6:8
2. Omba Mungu atume watenda kazi katika shamba lake kwani waliopo ni wachache, Luka 10:2
• Baadhi wanatoa udhuru, na kuchelewesha ukuaji wa kanisa John 9:4, Mathayo 21:28-30
• Baadhi wana wito ila hawana uhakika wachukue hatua gani hivyo wanaogopa kutoka. Omba Mungu athibitishe wito wake kwao na awajaze ujasiri. Waamuzi 6:39, Ezra 10:4
3. a) Omba watu wajitoe kikamilifu kumtumikia Mungu kwa nafasi ambazo wanasukumwa kutumika. Yeremia 48:10.
– Omba Mungu akuwezeshe kutoa fedha kwa umisioni na kupanda makanisa. . 2 Nyakati 33:17
b) Omba kwa ajili ya watenda kazi waliopo ili Mungu aendelee kuwalinda na kuwapatia mahitaji yao. Waombee kibali, ujasiri na umoja. 2Wathesalonike 3:1-2, 1 Wakorintho 16:19, 9:7, Wagalatia 2:9
4. Omba Idara ya Uinjilisti na Umisheni kuanzia ngazi ya Taifa hadi kanisa la mahali ipate rasilimali watu na fedha ili kutimiza agizo kuu. Yoh 14:13-14
• Omba Mungu awaguse watu wake kutoa fedha / vifaa husika kwa ajili ya Injili. Warumi 10:15. – Hagai 2:8