Maono: Kuwa kanisa la kimataifa linalokua ki idadi na ki ubora.
Dira: Kuwafanya watenda dhambi wawe watakatifu na kuwaongoza kumwabudu Mungu katika Roho na Kweli; kuwasaidia kujitoa kwa kanisa la mahali; kuwakuza katika tabia ya Kristo na kuwajenga kutumia vipawa walivyopewa na Mungu kutumika katika huduma ndani na nje ya nchi.
Ili kufikia malengo hayo, DPC itakuwa kanisa la vikundi vidogo vidogo yaani seli. Kwenye vikundi vidogo vidogo ndiko ambako mabadiliko hutokea.
Je Seli ni nini?
Seli ni kikundi kidogo cha watu kati ya watano (5) hadi kumi na tano (15) wanaokutana kila wiki kwenye kusanyiko ambao si rasmi sana kujifunza neno na kuliweka katika matendo katika maisha ya kila siku. Kwenye seli ndiko watu hukua pamoja, huwa na ushirika wa pamoja, hutumika pamoja na kuwafikia wengine.
KUKUA– Kuwa mkristo unahitaji kuwa na mahusiano endelevu na Kristo (Mathayo 28:19-20). Kwenye seli ndiko washirika hufanyika kuwa wanafunzi wa Yesu na kukua kiroho.
USHIRIKA– Seli ni kikundi kidogo cha watu ambao huishi kwa kuhudumiana na kusaidiana.
HUDUMA– Seli ni sehemu ya kumhudumia Mungu na Kuhudumiana.
UINJILISTI– Utafiti unaonyesha kwamba zaidi ya asilimia 70% ya wakristo huja kwa Kristo kupitia marafiki. Seli inaweza kuwa chombo kizuri kwa ajili ya kuwafikia wengine na injili ya Kristo.
MAONO, DIRA NA MAADILI
Maono ya Huduma ya Seli : Kuwa Kanisa linaloendeshwa kwa mfumo wa seli, ambapo hakuna mtu anayesimama peke yake.
DIRA: kutengeneza jamii yenye mvuto, upendo na imani ambapo watu wanakutana na Mungu, wanahudumiana na wanafikia wengine na badiliko la kweli.
Maadili ya Msingi
1. Kukua Kiroho – tunahitaji kukua katika kumjua Mungu na Upendo wake huku tukiendelea kubadirishwa kufikia kima cha Kristo. (Warumi 12:1-2).
2. Kufikia Wengine – Tutakuwa watu wa kufikia wengine na injili ya Kristo. Tutaishi kukamilisha agizo kuu la utume (Mathayo 22:37-39; 28:19-20)
3.Kutumikiana – Tunataka kuona mahusiano halisi yaliyojengwa katika kutumikiana. Ni katika mahusiano haya ndipo, huduma ya kichungaji hutokea. (Matendo 2:46).
4.Kukuza Viongozi – Tutaendelea kuibua na kukuza viongozi kwa ajili ya Seli kwa dhumuni la kuwa na ongezeko endelevu. (Kutoka 18:21-23).