WIKI MBILI ZA KUFUNGA NA KUOMBA: DPC
11-23 January 2021
MAMBO YA KUOMBEA: JUMANNE 19/1/2021
- Kama watu waliookoka tuna wito wa kuombea watu wengine, familia, kanisa na mataifa. Omba ili Roho Mtakatifu akupe mzigo wa kuombea watu wengine, kanisa na mataifa. Warumi 8:26, Ezekieli 22: 30-31.
- Waombee watu wengine kadri Roho Mtakatifu anavyokuongoza. Ayubu 42:10, 1 Samweli 12: 23
• Ombea marafiki ambao hawajaokoka, wanafamilia na watu wengine kadri Roho Mtakatifu anavyokuongoza. Omba dhidi ya roho zinazowazuia kupokea wokovu. Omba neema ya kupokea wokovu. Yohana 3:16, 1 Timotheo 2: 3-4, Matendo 26:18, 2 Wakorintho 4: 4.
• Ombea watu wengine wenye mahitaji tofauti tofauti hata wale ambao ni maadui zako. Yakobo 5: 16
• Waombee wachungaji wako na familia zao na watumishi wa Mungu wengine. Omba kwamba Mungu awabariki, awatie nguvu na awalinde. 2 Wakorintho 1:11
- Omba kwa ajili ya taifa la Tanzania na mataifa mengine.
• Tubu kwa niaba ya taifa lako kama unavyoongozwa na Roho Mtakatifu. Omba Mungu akusamehe na kuiponya nchi yako. Omba Ufalme wa Mungu utawale katika taifa lako. 2 Nyakati 7: 14-15
• Waombee viongozi wa Serikali. Ombea hekima na hofu ya Mungu. Omba amani na ulinzi juu ya nchi yako. 1 Timotheo 2: 1-2, Zaburi 22: 27-28, Mathew 6: 10
• Tamka Baraka za Mungu juu ya taifa lako.
- Mshukuru Mungu na utangaze kusudi la Mungu kutawala Tanzania na mataifa yote ya ulimwengu. Zaburi 97: 1-6