WIKI MBILI ZA KUFUNGA NA KUOMBA: DPC
11- 23 Januari 2021
MAMBO YA KUOMBEA: JUMATATU: 11/1/2021
- Mshukuru Mungu kwa uaminifu wake katika mwaka 2020. Mshukuru kwa Kumsifu na kumuabudu na maombi; kwa ajili ya neema yake, kibali, upaji, ulinzi na mambo yote ambayo ameyafanya maishani mwako. Zaburi 28: 7; 100: 4-5; 107: 8-9, 1 Wakorintho1: 4
- Jiweke wakfu kwa Bwana na kabidhi siku zote za maombi na kufunga. Yoshua 3: 5
•Omba Roho Mtakatifu atusaidie katika maombi yetu ili tuweze kuomba kulingana na mapenzi ya Mungu. Warumi 8:26-27
•Omba udhihirisho wa nguvu za Mungu kila siku tunapomtafuta. Matendo 4:31 - Omba kinyume na pepo wachafu na nguvu za giza zilizojipanga kukuzuia kuomba kwa ufanisi. Omba kinyume na roho za magonjwa, uzito na vitu vyote vinavyoweza kusababisha usumbufu.
Mathayo 18: 18-19, 1 Petro 5: 8-9. - Mshukuru Mungu kwa ajili ya upako na uhuru wa kuomba. Mshukuru Mungu kwa udhihirisho wa utukufu wake katikati yetu tunapoutafuta uso wake.
2 Wakorintho 3: 17-18