Mungu anakupenda na alikuumba ili umjue yeye Upendo wa Mungu “ Kwa Maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa mwanae wa pekee, ili kila amwaminie asipotee bali awe na Uzima wa milele ” Yohana 3:16 .
Mpango wa Mungu “Na huu ndio uzima wa milele: wakufahamu wewe ambaye pekee ni Mungu wa kweli, nakumfahamu Yesu Kristo ambaye umemtuma.”(Yohana 17:3 ).
“ Na ushuhuda wenyewe ndio huu: Mungu ametupatia uzima wa milele, na uzima huu umo kwa Mwanae. Aliye naye Mwana anao uzima; asiye naye Mwana wa Mungu hana uzima.” 1 Yohana 5:11-12
Je ni kitu gani kinazuia sisi tusimjue Mungu? “Dhambi zimetutenga na Mungu wetu”
2. Mwanadamu ni Mwenye dhambi na amejitenga na Mungu, Hivyo hawezi kumjua Mungu au kuujua upendo wa Mungu.
Mwanadamu ni Mwenye dhambi
“kwa maana wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu” (Warumi 3:23). Mwanadamu aliumbwa ili awe na mahusiano na Mungu, ila
kutokana na usumbufu wake akaamua kwenda njia yake na uhusiano na Mungu ukavunjika. Uwezo wa kuamua wa mwanadamu ukaleta tabia ya uasi au kutofautiana na Mungu na hichi ndicho Biblia inasema kuwa ni dhambi.
Mwanadamu Ajitenga “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti, bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu (Warumi 6:23). “…
(Wale ambao hawamjui) Atawahukumu wale wasiomjua Mungu, wasioitii Habari Njema ya Bwana wetu Yesu. 9 Wata- adhibiwa kwa kuangamizwa milele na kutengwa na uso wa Bwana na utukufu wa nguvu zake.” (2 wathesalonike 1:8,9)
3. Yesu Kristo ni Msaada wa Mungu kwa Wanadamu wenye dhambi. Kupitia yeye, tunaweza kumjua Mungu binafsi na kujua upendo wake.
Yesu alikufa kwa ajili yetu
Alikufa kwa ajili yetu “Lakini Mungu anaudhihirisha upendo wake kwetu kwamba: tulipokuwa tungali wenye dhambi, Kristo ali kufa kwa ajili yetu.” (Warumi 5:8).
Alifufuka kutoka katika wafu” Kwa maana niliyopokea ndio niliyowapa ninyi, nayo ni muhimu sana: kwamba Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama ilivyoandikwa katika Maandiko. Na kwamba alizikwa na kufufuka siku ya tatu, kama ilivyoandikwa katika Maandiko. Na kwamba alimto kea Kefa, kisha akawa- tokea wale kumi na wawili. Baadaye akawa tokea ndugu waamini zaidi ya mia tano kwa pamoja, na wengi wao wangali hai, ingawa wengine wameshakufa.” (1 Wakorintho 15:3-6). “Yesu akawaambia,“Mimi ndiye Njia na Baba bila kupitia kwangu.'” (Yohana 14:6).
Yesu akawaambia,“Mimi ndiye Njia na Baba bila kupitia kwangu.’
4.Tunatakiwa kumpokea Yesu awe Bwana Na Mwokozi wa Maisha Yetu, Ndipo tuweze kumjua Mungu na Kuujua Upendo wake.
“Bali wote waliompokea na kumwamini aliwapa haki ya kufanywa watoto wa Mungu” (Yohana 1:12)
Tunampokea Yesu kwa Imani “Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; na si kwa sababu ya matendo yenu mema. Hii ni zawadi kutoka kwa Mungu mwenyewe. Na kwa sababu hamkuifanyia kazi, mtu ye yote asije akajisifu juu ya wokovu wake”
(Waefeso 2:8,9). Tunapompokea Yesu Kristo, Tunazaliwa Upya (Yohana 3:1-8.)