MUONGOZO WA KUOMBEA IBADA YA KUSIFU NA KUABUDU YA MWISHO WA MWEZI- APRILI 2021.

Andiko kuu: Zaburi 145
(mahali popote utakapotajwa mstari(vs) bila kutaja kitabu utarejelea andiko kuu)

  1. MHIMIDI NA KUMSIFU MUNGU
    • Msifu Mungu kwa jinsi alivyo, tambua uweza na ukuu wake, mshukuru na utangaze matendo yake makuu na ya kutisha, mshukuru kwa uaminifu na wema wake; (vs 1-13,21) kwako binafsi, familia yako, kanisa na taifa.
    • Eleza wazi, (sio kijumlajumla), taja kila kitu unachoweza kumshukuru na kumsifu Mungu kwacho (Msifu kwa nyimbo, kucheza, ala, makofi, na umaanishe. Zaburi 150)
  2. TUBU NA KUJIWEKA WAKFU. vs 8-9
    • Tubu dhambi zote unazozijua (taja moja moja na umruhusu Roho Mtakatifu auchunguze moyo wako na kukusemesha, tubu kwa dhati) 1Yohana 1:8-10, Zaburi 139:23-24.
    • Omba rehema kwa Mungu (tunahitaji rehema za Mungu, usijihesabie haki hata kama unaweza kushuhudia kwamba una mahusiano mazuri na Mungu), kwa maana Yeye tu ndiye anayetuhesabia haki. Warumi 3:23; 5:9
    • Tubu kwa niaba ya timu yako, wote watakaohudumu na kusanyiko zima.
  3. MAANDALIZI NA IBADA YENYEWE.
    • Omba kutiwa nguvu. Jiombee mwenyewe, wanakikundi chako cha huduma, familia yako na wote watakaohudumu . Omba kinyume na roho za magonjwa, vifo, ajali, kufarakana, na kitu chochote ambacho kinaweza kuleta usumbufu(vs 20), jifunike kwa damu ya Yesu(Waebrania 12:24).
    • Muombe Roho Mtakatifu aufunue kwetu moyo wa Baba, tuweze kujua mapenzi yake makamilifu na mpango wake juu ya ibada hii, ili tuweze kuomba sawa sawa. Rum 8:26-27
    • Omba kwamba Roho Mtakatifu atawale kila kitu kinachohusu huduma tunapojiandaa na kupanga, na tusifanye chochote kwa mazoea, uzoefu wala kutimiza wajibu.
    • Ombea mnenaji wa neno, Mungu ampe neno la wakati na majira na kwamba atanena mawazo ya Mungu na hekima itokayo juu. Gal 1:11-12, Muombee anene kwa ujasiri na kwa ufunuo.
    • Omba kwamba nguvu
    ya Neno ibadilishayo itashughulika kibinafsi na moyo wa kila msikilizaji (wote watakaokuja na wale watakaoabudu kwa njia ya mtandao) Waebrania 4:12-13, Mdo 2:37
    • Omba kwamba hii itakuwa ibada ya upenyo na watu watapokea majibu ya maombi yao, suluhisho kwa matatizo yao, maono na mawazo yatazaliwa, ahadi za Mungu zilizosubiriwa kwa muda mrefu zitatimia na haja za mioyo ya watu wa Mungu zitajibiwa (vs 14- 19).
    • Ombea mahudhurio, omba kwamba kila mtu ambaye Mungu amemkusudia atakuja. Omba kwamba njia zote za kufikisha taarifa kuhusu ibada hii zitaleta matokeo mazuri (kwa mdomo, vyombo vya habari, mitandao ya kijamii nk)
  4. MSHUKURU MUNGU NA KUTAMKA NENO LAKE
    • Msifu na kumshukuru Mungu kwa imani kwa kile ulichoombea 1Yohana 5:14-15.
    • Tangaza uaminifu wa Mungu na umshukuru (vs 14,17), 2Tim 2:13
    • Tangaza baraka za Mungu juu yako mwenyewe, familia, kanisa na taifa. Hesabu 6:24-26. Mshukuru kwa kuwa atakupa mahitaji yako yote Phil 4:19
    • Tangaza na umshukuru Mungu, mpiganaji wa vita yako kwa maana hatakuacha uangukie mikononi mwa adui zako wala kumruhusu adui akushinde wewe, familia yako, kanisa, wala taifa letu Tanzania.
    Zaburi 144:1-2; 25:2
    • Mkiri Kristo aliye amani yetu na tangaza kwamba Mungu atakupa amani kila upande na yote yanayokuhusu. Isaya 9:6, 1Wafalme 5:4.

Join the Discussion

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top