A. SHUKRANI NA SIFA KWA MUNGU (1 Nya 16:7-9, Zab 95:1-6; 34:1-3, 2 Kor 2:14.)
● Mshukuru Mungu:-
~ Kwa ajili ya wema wake na uaminifu wake kwako na wote wanaokuzunguka.
~ Ushindi aliotupa katika nusu hii ya kwanza ya mwaka, kibinafsi na kama kanisa (Januari hadi Juni).
~ Kwa neema, upendo, fadhili, wema na rehema zake juu ya kanisa letu.
~ Kwa ajili ya huduma unayohudumu kanisani (Kumpenda Mungu, nguvu ya kutumika, umoja na amani katika timu yako).
B. TOBA NA UTAKASO (Mit 28:13, Zab 32:5; 139:23-24, Ufu 5:9-10.)
● TUBU
~ Muombe Roho Mtakatifu auchunguze moyo wako na akusemeshe juu ya dhambi yoyote inayokupasa kuitubia.
~ Mahali tulipomtumikia chini ya viwango.
~ Tubu kwa niaba ya timu yako, wote watakaohudumu, kanisa na kusanyiko zima.
~ Mshukuru Mungu kwa msamaha na rehema zake kwetu.
C. HUDUMA NZIMA (Zab 40:8; 32:8, 1 Sam 15:22, 2 Sam 5:3, Isa 40:29, Mdo10:38.)
● KWA AJILI YAKO NA WOTE WATAKAOHUDUMU
☆ OMBA;
~ Roho Mtakatifu akufunulie kusudi na mapenzi yake kwa ajili ya ibada.
~ Maelekezo na uongozi wa Roho Mtakatifu katika maandalizi yetu.
~ Neema ya kumtumikia kwa uaminifu na ufanisi.
~ Nguvu; kiroho, kimwili, kiakili na kihisia.
~Upako mpya na wa kiwango kingine uwe juu yetu, Bwana anavyotutumia kufanya kile alichokikusudia katika ibada hii.
~ Moyo wenye kutii sauti ya Roho Mtakatifu ili tukae katika mapenzi yake wakati wote wa huduma.
~ Umoja katika roho.
● MNENAJI WA NENO (Isaya 40:8, Luka 24:45; 22:42b na 4:14, 22, 32.)
☆ OMBEA:-
~ Mnenaji kubeba ajenda ya Mungu na kutoa neno la wakati.
~ Mamlaka, ujasiri na ufasaha katika kulinena neno.
~ Tamka, utimilifu wa neno la Mungu na kusudi lake kwa wale watakaolisikia; liguse maisha, hali zao na mambo wanayoyapitia.
● KUSANYIKO (Yer 30:19, Ebr 11:1-2 na 6, Mdo 2:1-2, 2 Nya 5:13.)
☆ OMBEA:-
~ Mioyo iliyojaa shukrani kwa Mungu kwa yote aliyofanya katika nusu hii ya kwanza ya mwaka, na yale ambayo bado hajafanya.
~ Imani ya kupokea kile ambacho wamekuwa wakimwamini Mungu kuwatendea na matarajio yao kwa nusu ya pili ya mwaka.
~ Udhihirisho wa uwepo wa Mungu, upako na nguvu za Roho Mtakatifu ili kutimiza kusudi la kila mtu binafsi katika miezi sita ijayo.
D. KIRI NA KUTANGAZA (Isa 2:3, Yoh 4:28-30, Luka 4:18 &19, 2Kor 10:4-5, Isa 54:14-17, Zab 91.)
Tamka:-
~ Mahudhurio; mitandao ya kijamii na njia nyingine za kueneza habari; zibebe upako wa Roho Mtakatifu, na kwamba kila ambaye Mungu amemkusudia kuja atakuja, na wale watakaoabudu kwa njia ya mtandao watahudumiwa.
~ Juu ya wahudhuriaji wote;
☆ Wokovu
☆ Uponyaji
☆ Upenyo
☆ Kufunguliwa
☆ Urejesho
☆ Uamsho
~ Damu ya Yesu ikufunike wewe na wapendwa wako wote tunapoendelea kujiandaa na ibada.
☆ Kila mpango wa adui na kila silaha itakayoinuka kinyume na wewe haitafanikiwa.
*Hakuna ugonjwa.
*Hakuna ajali.
*Hakuna kufa kabla ya wakati.