MWONGOZO WA MAOMBI; IBADA YA MWISHO WA MWEZI-SEPTEMBA 2022. MATOLEO YA BIBLIA (AMPC,NKJV, NIV, ESV, SUV, NENO). DHIMA: MSIMU WA KUZAA MATUNDA.
MISTARI YA BIBLIA: ISAYA 66:9 na YOHANA 15:8
1). TOBA (Zaburi 139:23-24, Yeremia 17:9-10)
● Nenda mbele za Bwana kwa Toba.
Mwombe Roho Mtakatifu auchunguze moyo wako na uziungame dhambi zote.
● Simama mahali palipobomoka kwa toba kwa ajili ya wahudumu wote, watakaohudumu katika ibada. 1 Samweli 12:23.
2). SHUKRANI KWA MUNGU WETU (Waefeso 5:20, Zaburi 100; 93)
● Chukua muda wa kumwinua Mungu na kumshukuru kwa jinsi alivyo. Mshukuru kwa uaminifu wake na kwa kila jambo analofanya katika maisha yako, familia, huduma, kanisa na taifa la Tanzania.
● Ombea maandalizi yote. Mithali 16:1-3
● Omba kuwa na bidii na kiu ya kutumika kwa moyo wote.
(Omba mahususi kwa ajili ya maeneo unayohudumu).
Zaburi 69:9 na Wakolosai 3:23-24.
3). IBADA NZIMA. (Zaburi 133).
● Omba UTUKUFU wa MUNGU ufunuliwe:-
~Katika maandalizi yote hadi siku ya ibada, watu wake wakimtafuta. Kutoka 33:13-21 na Yeremia 33:3.
~Kwa ajili ya wanaopitia nyakati ngumu/za taabu, waweze kustahimili mpaka mwisho. Warumi 8:18 na Yakobo 1:2-4.
~Na kuyadhihirisha mapenzi yake na makusudi ya moyo wake kwa ajili ya watu wake. Isaya 46:10 na Mathayo 6:9-10.
~Na kuwadhihirisha wana wa Mungu na karama za rohoni kwa ajili ya kulijenga Kanisa. Warumi 8:19 na
1 Wakorintho 12:1-11.
● Ombea upako wa Mungu juu ya maandalizi ya mnenaji.
~Omba neno la Mungu lifunuliwe upya kwake kwa ajili ya watu wake. Mithali 16:1-3 na Isaya 61:1-3.
Tangaza:- Neno la Mungu lizae na kutimiza kusudi lake.
1 Wathesalonike 1:5 na Mathayo 13:23.
● Ombea MAHUDHURIO, ili wengi waje kula mezani pa Bwana. (Mahudhurio ya ibada iliyopita hayakuwa mazuri).
4). VITA VYA KIROHO NA ULINZI. ( Waefeso 6:10-18 ).
● Mshukuru Mungu, tunashinda siku zote katika Kristo Yesu.
2 Wakorintho 2:14.
● Chukua muda kujifunza na kutafakari Maandiko haya; Waefeso 6:10-18, Wakolosai 2:15,
Waefeso 1:20-22; 2:6, Waebrania 2:14, 1 Yohana 3:8b, Yohana 14:12,
2 Timotheo 4:18; Luka 10:19;
2 Wakorintho 10:3-6,
Isaya 45:2-3.
● Omba Roho Mtakatifu akusaidie kutafuta maeneo ambayo shetani amechukua nafasi kinyume cha sheria katika maisha yako, nyumbani, huduma, kanisani. Omba kutoka katika nafasi ya USHINDI KAMILI. 1 Wakorintho 15:57.
Tumia mamlaka yako juu yake kwa kuomba dhidi ya:-
*Kucheleweshwa kwa baraka zako
*Kudumaa
*Mashambulizi katika ndoto
*Ukosefu wa kazi/ajira
*Utasa
*Magonjwa na maradhi
*Vifo vya mapema.
*Uraibu
*Kushindwa katika hatua ya mwisho ya mafanikio.
● Kiri na kutangaza:-
*Kwamba utazaa matunda mengi kwa ajili ya Ufalme wa Mungu. Wakolosai 1:9-10
*Milango ya kuzimu haitalishinda kanisa. Mathayo 16:18.
*Habari Njema ya Ufalme itahubiriwa hata miisho ya dunia.
Mathayo 28:18-19.
● Tamka (Zaburi 35:1-10; 91; 121) juu yako mwenyewe, familia, ROL, kazi, biashara, kusanyiko na DPC nzima.
TAFADHALI TENGA MUDA USOME KITABU CHA YOHANA 15:1-26.