1. SHUKRANI
Mshukuru Mungu kwa
~ Afya uliyo nayo
~ Upendo wake juu yako – Zaburi 92:1-2
~ Uongozi wa vijana na kanisa kwa ujumla kuandaa Youth baraza kwa lengo la kuwaelimisha vijana
~ Ajili ya Tanzania kutupa amani na utulivu licha ya kupita katika kipindi kigumu kama taifa, 1 Timotheo 2:1-2, 1 Wathesalonike 5:18
2 .TOBA
Tubu mbele za Mungu kwa
~ Niaba yako binafsi na vijana wengine kama Kuna mahali hatukuishi maisha ya utauwa Mungu atusamehe Zaburi 119:9
~ Kutokufuata maelekezo mbalimbali anayotupa, Luka 13:34, Mithali 5:13
3. MAANDALIZI
~ Ombea kila kitu kichopangwa kifanyike sawasawa mapenzi ya Mungu, Wakolosai 3:17
~ Ombea hali ya hewa iwe shwari
4. WANENAJI
~ Ombea utayari kwa wanenaji, 2 Timotheo 4:2
~ Ombea afya njema , hekima , ujasiri na kibali, Waefeso 6:20
~ Simama kinyume na kila kizuizi kinachoweza kusimama mbele yao, Warumi 16:9
5. Mshukuru Mungu kwamba amejibu maombi yetu na kiri neno lake kwamba atatupa akili katika mambo yote ya rohoni na mwilini, 2 Timotheo 2:7