MWONGOZO WA MAOMBI APRILI 2023.
DHIMA: NGUVU NA UFUNUO WA KAZI YA MSALABA. (WAKOLOSAI 2:14-15)
TAFSIRI ZA BIBLIA (NIV, NKJV, KJV, AMP, AMPC, SUV, NENO).
1). SHUKRANI KWA MUNGU WETU.
● Kwa ajili ya upendo wake, Rehema na Uaminifu. 1Yohana 4:19, Waefeso 2:4-5, Yohana 3:16.
● Mshukuru Mungu kwa kazi iliyokamilika ya MSALABA. Yohana 19:30.
Kupitia Msalaba…
~Tulipokea zawadi ya Wokovu (Uzima wa Milele)
~Nguvu ya dhambi, mauti na kaburi imevunjwa. Warumi 6:11,
1 Wakorintho 15:55 na Ufunuo 1:18.
~ Tumesamehewa, tumehesabiwa haki, tumetakaswa, tumekombolewa, tumefunguliwa na kupatanishwa naye.
~ Tumepona. Isaya 53:4-5.
~ Sisi ni washindi. Wakolosai 2:14-15, 1Wakorintho 1:18
~ Tumepata utambulisho mpya katika Kristo. Kanisa limepewa nguvu na mamlaka.
Waefeso 2:6.
~ Tumefanywa kuwa wafalme na makuhani, na tunamiliki na kutawala juu ya nchi.
(Ufunuo 5:9-10).
~Tunajifunza nguvu ya kudumu katika maombi (uwezo wa kukaa katika maombi hadi kuzaa kitu na kupata ushindi) na kuvumilia mpaka mwisho. Luka 22:39-46 .
2). TOBA NA HUDUMA.
(Jiombee na kuombea wengine hasa katika huduma unazotumika).
● Mkaribie Mungu kwa toba.
Omba damu yake ya thamani itusafishe, itufanye safi kwa ajili ya matumizi ya Bwana wetu.
Zaburi 24:3-4, 1Timotheo 2:8, Waebrania 9:14 na 2Timotheo 2:20-21.
● Tubu kwa niaba ya wahudumu wote na kusanyiko zima. Ufunuo 1:5-6.
●Jiombee na ukabidhi mahitaji yako kwake. Wafilipi 4:6. Mshukuru kwa sababu atatukumbuka na sisi tunapofanya kazi yake. Waebrania 6:10.
●Omba nguvu za kutumika, nguvu za Mungu zifanye kazi ndani yetu, hekima ya kutuongoza, kufanya kila kitu kwa ubora na kujitoa katika yote tunayofanya. Muhubiri 10:10, Waefeso 6:7-8.
● Tamka kwamba:- Tutafanya kazi alizofanya Kristo na zaidi. 1Yohana 3:8, Yohana 14:12.
3).IBADA NZIMA.
● Ombea:-
~Mioyo yenye matarajio, iliyojaa imani ya kupokea kutoka kwa Mungu. Marko 11:22-24.
~Watu wa Mungu wapate ufunuo mpya wa jina la YESU na JINA LA YESU linene na hali zao. Wafilipi 2:5-11, Matendo 4:12 ; 2:22 ; 3:1-16.
~ Watu wa Mungu wapate ufunuo mpya wa kazi iliyokamilika ya msalaba. 1 Wakorintho 1:18; 15:58, Wagalatia 3:13-14, Wakolosai 1:13-14.
~Mapenzi na kusudi la Mungu katika maandalizi yetu yote hadi siku ya mwisho.
Mathayo 6:10, Zaburi 135:6.
~ Udhihirisho wa uwepo wa Mungu na nguvu ya JINA LA YESU tunapokusanyika pamoja. Mathayo 18:20, Matendo 2:1-18, Luka 10:17.
~Ombea mnenaji wa neno.
*Mkabidhi Mungu maandalizi yote ya mnenaji. Mithali 16:1
*Omba upako wa kuhubiri neno. Usemi wake; Mungu ampe neno la majira kwa ajili ya watu wake nalo likatimize kusudi lake.
Omba wokovu wa roho na uamsho.
1 Wakorintho 1:4-5; 2:4-5, Luka 4:18-19.
*Ombea udhihirisho wa wana uamsho wa nyakati za mwisho ili kuhubiri Injili. Warumi 1:16, Mathayo 9:37-38.
● Tamka:
*MBINGU IMEFUNGUKA kwenye eneo la DPC. (Luka 3:21).
*Watu wengi waje kula mezani pa Mungu Jumapili hii na kusiwe na cha kuwazuia.
4). INUA JINA LA YESU KUPITIA SADAKA YA SIFA.
●Jina la Yesu linapoinuliwa kupitia dhabihu ya sifa, MWINULIE YESU SHANGWE:-
* Kwa ajili ya miujiza, ishara na maajabu. Matendo 2:22.
* Kwa uponyaji. Matendo 10:38
* Kufunguliwa.
* Kupigana vita yako. Zaburi 27:2-3.
* Kupigana na watesi wako. Zaburi 35:1
* Kwa urejesho.
* Kuokoa wapendwa wako. Mathayo 1:21.
● Kiri na kutamka kwamba;-
~Yesu anazo funguo za mauti na kuzimu (Ufu 1:18), kwahiyo milango ya kuzimu haitatushinda sisi, maandalizi yetu wala ibada. Mathayo 16:18.
~ Tamka Isaya 41:11-13, Zaburi 35:1-10 na 121, juu yako mwenyewe, timu yako ya huduma, wapendwa wako na ibada nzima.