MWONGOZO WA MAOMBI YA MWISHO WA MWEZI JULAI 2022.
MATOLEO YA BIBLIA (AMPC, NKJV, NIV, ESV, SUV, NENO).
DHIMA: PUMZIKA KWA BWANA.
MISTARI YA BIBLIA: YEREMIA 1:11-12 na MATHAYO 11:28-30.
1). MSHUKURU MUNGU, MWINULIE SIFA NA SHUKRANI.
(Zaburi 93:1-3; 138:1-3 ).
~Ni mwenye rehema na upendo. Zaburi 86:5
~Ni mwaminifu na wa kweli. 2Timotheo 2:13
~Yeye ni mkuu na mwenye nguvu
~Anastahili sifa zetu. Waebrania 13:15.
~ Yeye ndiye msaada wetu daima. Zaburi 46:1
~Yeye ndiye atushikaye na kututegemeza. Waebrania 1:1-3
~Anatamani ushirika nasi.
~ Mshukuru kwa ajili ya ibada zote zilizopita za sifa na kuabudu.
2). TOBA.
(Mika 6:6-8, Yeremia 17:9-10 na Zaburi 106:23 ).
● Tubu kwa ajili yako mwenyewe na kwa niaba ya wote watakaohudumu na kwa ajili ya kusanyiko lote.
● Mwombe Bwana achunguze mioyo yetu, afunue hali ya mioyo yetu na ungama dhambi zote.
A). MKABIDHI MUNGU MAANDALIZI YOTE.
( Mithali 16:3; 19:21 na Zaburi103:7).
Omba maalumu kwa ajili ya eneo unalotumika/unalohudumu.
Ombea:-
● Umoja katika roho na nia ya Kristo kufunuliwa wakati wa maandalizi na siku ya ibada. (Wakorinto 2:16).
● Mapenzi na makusudi yake yaonekane tunapomtafuta (Mathayo 6:10 na Zaburi 34:10b), Pia omba hekima, ufahamu, na mwongozo wake katika yote tunayofanya.
(Mithali16:16, Zaburi 32:8 & Isaiah 30:21).
● Moyo na nguvu za kumtumikia kwa moyo wote (Mathayo 20:27-28 na Isaiah 40:29-31).
3). IBADA NZIMA.
● Mshukuru Mungu kwa kuitenga DPC kama nyumba yake ya dhabihu (2Nyakati 7:1).
● Omba Mungu awashe moto upya katika madhabahu zetu binafsi na madhabahu ya pamoja tunapokusanyika kumwabudu.
Kiri na kutangaza kwamba:-
Moto utaendelea kuwaka wala hautazimika (Walawi 6:13).
Utukufu na uwepo wake vitadhihirika. (2Nyakati 5:11-14).
Tunapomtolea dhabihu zetu, ataketi katika hizo na kuzifurahia, nasi tutapokea baraka zake (waebrania 13:15, Zaburi 24:1-6; 84:11).
Moyo wa ibada, roho ya neema na kuomba, na maombezi na udhihirisho wa Roho Mtakatifu na nguvu zake ili kuwahudumia watu wake( Luka 18:1 ).
● Ombea mioyo yenye matarajio na iliyojaa imani kupokea kutoka kwa Bwana.
Tamka:-
Kuachiliwa kwa upako kwa ajili ya kasi na nguvu za kumaliza kwa nguvu katika miezi iliyobaki.(1Wafalme 18:46 na Wafilipi 4:13).
Kutakuwa na upenyo, shuhuda na unabii.
● Omba:-
Kwamba watu watakuja wakiwa na njaa na kiu ya kujazwa na Roho Mtakatifu. (Yohana 6:35, 7:37-39 na Matendo 2:1-4 ).
Kwa ajili ya kupokea karama za kiroho (Warumi 1:11 & Wakorinto 12:1-11), kwa huduma zote na kusanyiko zima.
Kwamba njia zote zinazotumiwa kuwafikia watu, zitaleta mahudhurio makubwa zaidi Jumapili hii (Ayubu 37:5).
A). MNENAJI WA NENO.
● Ombea:-
Neno na mnenaji wa neno, ili Roho wa Mungu akae juu yake kuanzia wakati wa maandalizi hadi siku ya ibada. ( Isaiah 11:2; 61:1-3 ).
Mamlaka, ufasaha na ujasiri wa kulisema neno la Mungu.
Neno la wakati kutoka kwenye moyo wa Mungu mwenyewe kwa ajili ya watu wake katika wakati na majira haya, na kwamba litatimiza kusudi ambalo limetumwa.
( 2Timotheo 3:16, Zaburi 119:130 & Isaiah 55:10-11 ).
Tangaza:-
Wokovu, uamsho, uponyaji, urejesho, pumziko mbali na vita nk.
4). VITA VYA KIROHO KWA NJIA YA SIFA NA KUTAMKA.
( Mithali 28:1, Zaburi27:1-6; 149 )
● Mwimbie Bwana na utamke na kukiri maandiko ya hapo juu kwa ujasiri, juu yako mwenyewe, wapendwa wako, huduma yako na kusanyiko zima.
TANGAZA:-
Ushindi wako dhidi ya mipango yoyote ya adui juu ya maandalizi yako, maombi na huduma yako. (Isaiah 54:13-17 na
Mathayo 16:18-19)
Mungu atafanya yale yanayompendeza katika ibada hii (Zaburi 115:3; 135:6).
● Mshukuru Mungu kwa kujibiwa maombi (Zaburi 66:19-20).