ITAKUWA HERI NA SALAMA KWAKO
ISAYA 3:10
Waambieni wenye haki ya kuwa watakuwa heri, kwa maana watakula matunda ya matendo yao
Kama itakuwa heri na salama kwetu, tufanye nini sasa (somo ktk ujumbe wetu)
- TUMPE MUNGU SHUKRANI
MAOMBOLEZO 3: 22 – 23
22. Ni huruma za Bwana kwamba hatuangamii, Kwa kuwa rehema zake hazikomi.
23. Ni mpya kila siku asubuhi; Uaminifu wako ni mkuu.
- Tumshukuru Mungu kwa ajili ya rehema zake zisizokoma kwetu kiasi kwamba hatuangamii
- Tumshkuru Mungu kwa ajili rehema zake ambazo ni mpya kila siku ili kututunza na kutuokoa
- Tumshukuru Mungu kwa ajili ya uaminifu wake kwetu
ZABURI 40: 1-3
1 Nalimngoja Bwana kwa saburi, Akaniinamia akakisikia kilio changu.
2 Akanipandisha toka shimo la uharibifu, Toka udongo wa utelezi; Akaisimamisha miguu yangu mwambani, Akaziimarisha hatua zangu.
3 Akatia wimbo mpya kinywani mwangu, Ndio sifa zake Mungu wetu. Wengi wataona na kuogopa, Nao watamtumaini Bwana
- Tumshukuru Mungu kwa sababu atatutoa katika shimo la uharibu na kutusimamisha mahali salama
- Tumshukuru Mungu kwa sababu anakwenda kuweka wimbo mpya katika vinywa vyetu (wimbo wa sifa)
2 TIMOTHEO 4: 16-18
Katika jawabu langu la kwanza hakuna mtu aliyesimama upande wangu, bali wote waliniacha; naomba wasihesabiwe hatia kwa jambo hilo. 17 Lakini Bwana alisimama pamoja nami akanitia nguvu, ili kwa kazi yangu ule ujumbe utangazwe kwa utimilifu, hata wasikie Mataifa yote; nami nikaokolewa katika kinywa cha simba. 18 Bwana ataniokoa na kila neno baya, na kunihifadhi hata nifike ufalme wake wa mbinguni. Utukufu una Yeye milele na milele. Amina.
- Tumshukuru Mungu kwa sababu anakwenda kusima upande wetu na kututia nguvu
- Tumshukuru Mungu kwa sababu anakwenda kutuokoa dhidi ya adui
- Tumshukuru Mungu kwani atatuongoza ili tufikie ufalme wake