KNOW JESUS AND BELIEVE IN HIM – MJUE YESU NA UMWAMINI

MJUE YESU NA UMWAMINI
[KNOW JESUS AND BELIEVE IN HIM]

YESU NI NANI? WHO IS JESUS?
YOHANA 20:30-31

  1. MTUME YOHANA AMEMTAMBULISHA YESU
    [YOHANA 1:1-18]

I. YESU NI MUNGU (JESUS IS GOD)

II. NENO AKAFANYIKA MWILI [THE WORD BECAME FLESH]

ALIKUJA NA NEEMA NA KWELI
Yohana 1:14

ALIMFUNUA MUNGU WA KWELI

  1. YESU ANAJITAMBULISHA [JESUS INTRODUCES HIMSELF]

MIMI NI MKATE WA UZIMA. [I AM THE BREAD OF LIFE.]
Yohana 6:35

MIMI NI NURU YA ULIMWENGU [I AM THE LIGHT OF THE WORLD]
Yohana 8:12

MIMI NDIMI MLANGO WA KONDOO [I AM THE DOOR OF THE SHEEP]

MIMI NI MCHUNGAJI MWEMA. [I AM THE GOOD SHEPHERD]
Yohana 10:11,14

MIMI NDIMI UFUFUO NA UZIMA. [I AM THE RESURRECTION AND THE LIFE]
Yohana 11:25

MIMI NDIMI NJIA NA KWELI NA UZIMA. [I AM THE WAY, THE TRUTH, AND THE LIFE]
Yohana 14:6

MIMI NDIMI MZABIBU WA KWELI. [I AM THE TRUE VINE]
Yohana 15:1-2

MIMI NI ALFA NA OMEGA, MWANZO NA MWISHO. [I AM ALPHA AND OMEGA THE BEGINNING AND THE]
Ufunuo 1:8

YOHANA 20:30-31

  1. Basi kuna ishara nyingine nyingi alizozifanya Yesu mbele ya wanafunzi wake, zisizoandikwa katika kitabu hiki.
  2. Lakini hizi zimeandikwa ili mpate kuamini ya kwamba Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini mwe na uzima kwa jina lake

YOHANA 1-18

  1. Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.
  2. Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu.
  3. Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika.
  4. Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu.
  5. Nayo nuru yang’aa gizani, wala giza halikuiweza.
  6. Palitokea mtu, ametumwa kutoka kwa Mungu, jina lake Yohana.
  7. Huyo alikuja kwa ushuhuda, ili aishuhudie ile nuru, wote wapate kuamini kwa yeye.
  8. Huyo hakuwa ile nuru, bali alikuja ili aishuhudie ile nuru.
  9. Kulikuwako Nuru halisi, amtiaye nuru kila mtu, akija katika ulimwengu.
  10. Alikuwako ulimwenguni, hata kwa yeye ulimwengu ulipata kuwako, wala ulimwengu haukumtambua.
  11. Alikuja kwake, wala walio wake hawakumpokea.
  12. Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake;
  13. waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu.
  14. Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.
  15. Yohana alimshuhudia, akapaza sauti yake akasema, Huyu ndiye niliyenena habari zake ya kwamba, Ajaye nyuma yangu amekuwa mbele yangu; kwa maana alikuwa kabla yangu.
  16. Kwa kuwa katika utimilifu wake sisi sote tulipokea, na neema juu ya neema.
  17. Kwa kuwa torati ilitolewa kwa mkono wa Musa; neema na kweli zilikuja kwa mkono wa Yesu Kristo.
  18. Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote; Mungu Mwana pekee aliye katika kifua cha Baba, huyu ndiye aliyemfunua.

Yohana 1:14
Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.

John 6:35
6:35 Yesu akawaambia, Mimi ndimi chakula cha uzima; yeye ajaye kwangu hataona njaa kabisa, naye aniaminiye hataona kiu kamwe.

35 Then Jesus declared, ìI am the bread of life. Whoever comes to me will never go hungry, and whoever believes in me will never be thirsty. NIV

8:12 Basi Yesu akawaambia tena akasema, Mimi ndimi nuru ya ulimwengu, yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima.

JOHN10:7-8
7 Basi Yesu aliwaambia tena, Amin, amin, nawaambieni, Mimi ndimi mlango wa kondoo.

8 Mimi ndimi mlango; mtu akiingia kwa mimi, ataokoka; ataingia na kutoka, naye atapata malisho.

Yohana 10:11,14

  1. Mimi ndimi mchungaji mwema. Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo
  2. Mimi ndimi mchungaji mwema; nao walio wangu nawajua; nao walio wangu wanijua mimi;

Yohana 11:25
25 Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi;

Yohana 14:6
6 Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.

Yohana 15:1-2
1 Mimi ndimi mzabibu wa kweli, na Baba yangu ndiye mkulima.

2 Kila tawi ndani yangu lisilozaa huliondoa; na kila tawi lizaalo hulisafisha, ili lizidi kuzaa

Ufunuo 1:8
8 Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, asema Bwana Mungu, aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja, Mwenyezi.

×Note: To download, click the button. If it doesn't work, right click, then click "Save Link As." Download only works if media is stored within this site. Download Video

Join the Discussion

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top