NINI MAANA YA KUMSHURU MUNGU?
Ni kumpa shukrani Mungu kutoka Moyoni kwa njia ya maneno, Maombi, nyimbo na vitu
ZABURI 50:14 Mtolee Mungu dhabihu za kushukuru; Mtimizie Aliye juu nadhiri zako.
ZABURI 118: 1-4 Haleluya. Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema, Kwa maana fadhili zake ni za milele. Israeli na aseme sasa, Ya kwamba fadhili zake ni za milele. Mlango wa Haruni na waseme sasa, Ya kwamba fadhili zake ni za milele. Wamchao Bwana na waseme sasa, Ya kwamba fadhili zake ni za milele.
KUTOA SHUKRANI NI AGIZO
- MSHUKURU MUNGU KWA ALIYO KUTENDEA
ZABURI 116:12,17 Nimrudishie Bwana nini Kwa ukarimu wake wote alionitendea? 17 Nitakutolea dhabihu ya kushukuru; Na kulitangaza jina la Bwana
2 NYAKATI 5:12-14 tena Walawi waimbaji, wote pia, yaani Asafu, na Hemani, na Yeduthuni, na wana wao, na ndugu zao, hali wamevaa kitani safi, wenye matoazi na vinanda na vinubi, wamesimama upande wa mashariki wa madhabahu, na pamoja nao makuhani mia na ishirini wakipiga panda;) hata ikawa, wenye panda na waimbaji walipokuwa kama mmoja, wakisikizisha sauti moja ya kumsifu na kumshukuru Bwana nao wakipaza sauti pamoja na panda na matoazi na vinanda, wakimsifu Bwana, wakisema, Kwa kuwa ni mwema; kwa maana fadhili zake ni za milele; ndipo nyumba ikajawa na wingu, naam, nyumba ya Bwana, hata makuhani hawakuweza kusimama ili kufanya huduma yao, kwa sababu ya lile wingu; kwa kuwa nyumba ya Mungu imejaa utukufu wa Bwana
- MSHUKURU MUNGU KWA AJILI YA ANAYO YATENDA KATIKA MAISHA YAKO.
MAOMBOLEZO 3:22-23 Ni huruma za Bwana kwamba hatuangamii, Kwa kuwa rehema zake hazikomi. Ni mpya kila siku asubuhi; Uaminifu wako ni mkuu.
KILA SIKU MSHUKURU KWA AJILI YA WEMA WAKE
EZRA 3:10-13 Hata wajenzi walipouweka msingi wa hekalu la Bwana, wakawaweka makuhani, wamevaa mavazi yao, wenye baragumu, na Walawi, wana wa Asafu, wenye matoazi, ili wamhimidi Bwana, kama alivyoagiza Daudi, mfalme wa Israeli. Wakaimbiana, wakimhimidi Bwana, na kumshukuru, wakasema, Kwa kuwa ni mwema, kwa maana fadhili zake kwa Israeli ni za milele. Kisha watu wote wakapaza sauti zao, na kupiga kelele, walipomhimidi Bwana, kwa sababu msingi wa nyumba ya Bwana umekwisha kuwekwa. Bali makuhani wengi, na Walawi, na wakuu wa mbari za mababa, waliokuwa wameiona nyumba ya kwanza, wakati msingi wa nyumba hii ulipowekwa mbele ya macho yao, walilia kwa sauti kuu; na watu wengi walipiga kelele za furaha; hata watu wasiweze kupambanua kelele za furaha, na kelele za vilio vya watu; maana watu walipiga kelele kwa sauti kuu, na kelele zao zikasikilikana mbali sana.
- MUSHUKURU MUNGU KWA ANAYOKWENDA KUYAFANYA KATIKA MAISHA YAKO
1 WAKORINTHO 15:57 NKJV Lakini Mungu na ashukuriwe atupaye kushinda kwa Bwana wetu Yesu Kristo.
DANIEL 6:10-12 NIV
Hata Danieli, alipojua ya kuwa yale maandiko yamekwisha kutiwa sahihi, akaingia nyumbani mwake, (na madirisha katika chumba chake yalikuwa yamefunguliwa kukabili Yerusalemu;) akapiga magoti mara tatu kila siku, akasali, akashukuru mbele za Mungu wake, kama alivyokuwa akifanya tokea hapo. Basi watu hao wakakusanyika pamoja, wakamwona Danieli akiomba dua, na kusihi mbele za Mungu wake.
Ndipo wakakaribia, wakasema mbele ya mfalme katika habari ya ile marufuku ya mfalme; Je! Hukuitia sahihi ile marufuku, ya kwamba kila mtu atakayeomba dua kwa Mungu awaye yote, au kwa mtu awaye yote, katika muda wa siku thelathini, ila kwako, Ee mfalme, atatupwa katika tundu la simba? Mfalme akajibu, akasema, Neno hili ni kweli, kama ilivyo sheria ya Wamedi na Waajemi isiyoweza kubadilika.
KATIKA KILA JAMBO MPE MUNGU SHUKRANI
WAFILIPI 4:6-7
Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.
Yona 2:7-10 ESV Roho yangu ilipozimia ndani yangu, Nalimkumbuka Bwana; Maombi yangu yakakuwasilia, Katika hekalu lako takatifu. Watu waangaliao mambo ya ubatili na uongo Hujitenga na rehema zao wenyewe; Lakini mimi nitakutolea sadaka kwa sauti ya shukrani; Nitaziondoa nadhiri zangu. Wokovu hutoka kwa Bwana. Bwana akasema na yule samaki, naye akamtapika Yona pwani.
HITIMISHO
MPE BWANA SHUKRANI