POKEA UWEZA WA KI MUNGU KWA AJILI YA HATIMA YAKO
2 PETRO 1:3-4 Kwa kuwa uweza wake wa Uungu umetukirimia vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa, kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe.
2Pe 1:4 Tena kwa hayo ametukirimia ahadi kubwa mno, za thamani, ili kwamba kwa hizo mpate kuwa washirika wa tabia ya Uungu, mkiokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa.
- Nguvu ya Kiungu hutoka kwa Roho mtakatifu
- Nguvu ya Kiungu imetukirimia vitu vyote vipavyo uzima na utaua
- Kupitia nguvu ya Ki Mungu tunakwa washirika wa tabia ya Ki Mungu.
- Nguvu ya ki Mungu hutuwezesha kuishi maisha ya ushindi.
- Tunahitaji nguvu ya Ki Mungu kutimiza kusudi la Mungu hapa duniana.
KUTIWA NGUVU NA ROHO MTAKATIFU
- JAZWA NGUVU ZA ROHO MTAKATIFU
MATENDO 1:4-5
1:4 Hata alipokuwa amekutana nao aliwaagiza wasitoke Yerusalemu, bali waingoje ahadi ya Baba, ambayo mlisikia habari zake kwangu;
1:5 ya kwamba Yohana alibatiza kwa maji, bali ninyi mtabatizwa katika Roho Mtakatifu baada ya siku hizi chache.
1:8 Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.
- Yesu alisema mstoke mpaka mmepokea nguvu za Roho mtakatifu
- Ndipo mtaweza kuwa mashahidi wangu.
- Mtaweza kushinda
MATENDO 2:1-4
ct 2:1 Hata ilipotimia siku ya Pentekoste walikuwako wote mahali pamoja.
Act 2:2 Kukaja ghafula toka mbinguni uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza nyumba yote waliyokuwa wameketi.
Act 2:3 Kukawatokea ndimi zilizogawanyikana, kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao.
Act 2:4 Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka.
- Roho mtakatifu aliwajaza nguvu za Ki Mungu ms e
- Ujazo wa Nguvu za Roho mtakatifu . Matendp 2:38-39
ct 2:38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.
Act 2:39 Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie.
- Unapojazwa nguvu za Roho Mtaktifu, ROHO MTAKATIFU HUKUSAIDIA KUABUDU katika roho na kweli. Ms 2:11
- Walipo jazwa nguvu za Roho mtaktifu walinena kwa lugha mpya
- Unapo omba kwa lugha mpya unaongea na Mungu
- Unaongea mambo ya siri katika roho yaka
- Hujijenga nafsi yake
- Walipojazwa nguvu za Roho mtakatifu maisha yao yalibadiliswa,
- ONGOZWA NA ROHO MTAKATIFU
ROMANS 8:13-14
Rom 8:13 kwa maana kama tukiishi kwa kufuata mambo ya mwili, mwataka kufa; bali kama mkiyafisha matendo ya mwili kwa Roho, mtaishi.
Rom 8:14 Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu.
- Wana wa Mungu huongozwa na Roho Mtakatifu hawaongozwi
- Wote walio mpokea Yesu wamefanyika watoto wa Mungu, wamezaliwa Kwa Roho Mtkatifu.
- Roho mtaktifu huwapa nguvu ya kushinda dhambi, hawako tena chini ya sharia ya dhambi.
TUMEPEWA NGUVU YA KUSHINDA DHAMBI
Rom 8:1 Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu.
Rom 8:2 Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti.
ISHI KWA KUFUATA MATAKWA YA ROHO MTAKATIFU
Wagalatia 5:16 Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili.
Wagalatia 3:24-25
Gal 5:24 Na hao walio wa Kristo Yesu wameusulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake.
Gal 5:25 Tukiishi kwa Roho, na tuenende kwa Roho.
- TUMIWA NA ROHO MTAKATIFU
Matendo 6:3
Act 6:3 Basi ndugu, chagueni watu saba miongoni mwenu, walioshuhudiwa kuwa wema, wenye kujawa na Roho, na hekima, ili tuwaweke juu ya jambo hili;
Matendo 6:5-6
ct 6:5 Neno hili likapendeza machoni pa mkutano wote; wakamchagua Stefano, mtu aliyejaa imani na Roho Mtakatifu, na Filipo, na Prokoro, na Nikanori, na Timoni, na Parmena, na Nikolao mwongofu wa Antiokia;
MATENDO 6:8
Act 6:5 Neno hili likapendeza machoni pa mkutano wote; wakamchagua Stefano, mtu aliyejaa imani na Roho Mtakatifu, na Filipo, na Prokoro, na Nikanori, na Timoni, na Parmena, na Nikolao mwongofu wa Antiokia;
- Roho Mtakatifu hutupa uwezo wa kufanya mambo Zaidi ya uwezo wa Kibinadamu
- Hutupa karama za kiroho ili tutumike kwa kiwango cha Ki Mungu
ROHO MTAKATIFU HUTUPA NGUVU ZA KUTUWEZESHA KUSHINDA CHANGAMOTO NA VIZUIZI
MATENDO 13:6-12
ct 13:6 Walipokwisha kupita katikati ya kisiwa chote mpaka Pafo, wakaona mtu mmoja, mchawi, nabii wa uongo, Myahudi jina lake Bar-Yesu;
Act 13:7 mtu huyu alikuwa pamoja na liwali Sergio Paulo, mtu mwenye akili. Yeye liwali akawaita Barnaba na Sauli waje kwake, akataka kulisikia neno la Mungu.
Act 13:8 Lakini Elima, yule mchawi (maana ndiyo tafsiri ya jina lake), akashindana nao, akitaka kumtia yule liwali moyo wa kuiacha ile imani.
Act 13:9 Lakini Sauli, ambaye ndiye Paulo, akijaa Roho Mtakatifu, akamkazia macho,
Act 13:10 akasema, Ewe mwenye kujaa hila na uovu wote, mwana wa Ibilisi, adui wa haki yote, huachi kuzipotoa njia za Bwana zilizonyoka?
Act 13:11 Basi, angalia, mkono wa Bwana u juu yako, nawe utakuwa kipofu, usilione jua kwa muda. Mara kiwi kikamwangukia na giza, akazunguka-zunguka na kumtafuta mtu wa kumshika mkono na kumwongoza.
Act 13:12 Ndipo yule liwali, alipoyaona yaliyotendeka, akaamini, akiyastaajabia mafundisho ya Bwana.
ROHO MTAKTIFU HUKUPA NGUVU YA KUHAMISHA MILIMA
Zakaria 4:6-7
ec 4:6 Akajibu akaniambia, akisema, Hili ndilo neno la Bwana kwa Zerubabeli, kusema, Si kwa uwezo, wala si kwa nguvu, bali ni kwa roho yangu, asema Bwana wa majeshi.
Zec 4:7 Nani wewe, Ee mlima mkubwa? Mbele ya Zerubabeli utakuwa nchi tambarare; naye atalileta lile jiwe la kuwekwa juu kabisa pamoja na vigelegele vya, Neema, neema, ilikalie.
POKEA NGUVU ZA ROHO MTAKATIFU
- Uwe na kiu ya kupokea
- Kama haujaoka mwamini yesu na umopokee kama mwokozi wa maisha yako.
- Uwe na Imani ya kwamba ukiomba utapokea
Download PDF