Siku 21 za Kufunga na Kuomba. (13 Januari 2024) Siku ya 6
HUDUMA ZA KIJAMII NA UINJILISTI
- Kila mshirika ajitoe kikamilifu katika kuwahudumia watu wengine.
Matendo 6: 1-7, Matendo 9:36 – 42, Wagalatia 6:9-10, Mithali 19:17, Yakobo 2:14-17.
– Mungu akuwezeshe kuwahudumia wahitaji ya watu wanaotuzunguka kwa mfano wazee, wagonjwa, wafungwa, watoto yatima nk. (Injili ya Matendo) - Ombea miradi ya kuwafikia watu na mahitaji yao hapa DPC na PAG kwa Ujumla.
Waefeso 1:17-19, Mithali 29:7, Kumb 15:11
– Ombea Mradi/Miradi ipate fedha na mahitaji mengine kwa ajili ya kufikia watu wengi zaidi inagusa
mahitaji ya watu na jamii kama NCCT n. k
– Ombea ubunifu, Kanisa liwe na ubunifu katika kuwafikia watu na mahitaji yao. - Tuombe kwa ajili ya huduma ya Uinjilisti hapa DPC. Mathayo 9:38, Mathayo 28:18-20
– Tuombe kwa ajili ya watenda kazi shambani mwa Bwana kwa ajili ya kuwafikia watu wengine na injili.
– Tuombee washirika tuwe na moyo wa kufanya uinjilisti (Mathayo 28:18-20),
– Tuombe kwa ajili ya Kila idara ibuni namna ya kufanya uinjilisti ili kuwafikia watu wa rika yao.
– Kanisa huihubiri injili ya kweli na kwa ufasaha. Waefeso 6:19-20 - Tuombe kwa ajili ya huduma ya Uinjilisti PAG Tanzania.
– Ombea watenda kazi wote kwenye idara hii kuanzia ngazi ya taifa hadi kwenye wilaya
– Ombea mipango ya uinjilisti mwaka huu ikafanikiwe na ikazae matunda
– Omba kwa ajili ya mahitaji ya huduma hii ili kufanikisha mipango yao