UMOJA, HESHIMA NA UTII.
DAR ES SALAAM PENTECOSTAL CHURCH
Siku 21 za Kufunga na Kuomba. (15 Januari 2024) Siku ya 8
UMOJA, HESHIMA NA UTII. 1 Yohana 4:20-21; Yohana 13:35; 2 Mambo ya Nyakati 30:12
- Uwe na roho ya upendo kwa Mungu, kwa watu wengine, kwa viongozi wa kanisa na serikali.
Warumi 12:16-18; 13:1-7; 2 Mambo ya Nyakati 30:12
Tuombe kwa ajili ya Upendo wa ndugu ndani ya kanisa na familia zetu. 1 Yohana 4:12
Kuwaheshimu watu wengine na kuwajali maana wote tumeumbwa kwa mfano wa Mungu. - Umoja katika kanisa la DPC. 1 Wakorintho 1:10; 3:1-3; 12:12-13, Waefeso 4:3,16
– Omba kila mmoja asimame katika nafasi yake. Warumi 12:4-5
– Ombea karama mbalimbali ndani ya kanisa. Waefeso 4:11-13 - Umoja katika Makanisa ya PAG na mwili wa Kristo. Waefeso 4:3,16;
– Ombea Umoja kuanzia ngazi Kanisa hadi juu katika kanisa la PAG Tanzania.
– Maana sisi zote tunategemeana tu viungo katika mwili kujenga kanisa imara. Zaburi 133:1 - Ombea Amani kwenye mataifa ambayo yamekubwa na machafuko, Vita na majanga mbalimbali.
– Mungu wa amani ashushe amani mashariki ya kati, Taifa la Israeli na Mataifa mengine dunianikote.
– Omba kwa ajili ya nchi ambazo wakristo hawana uhuru wa kuabudu ili Mungu aguse mioyo ya viongozi wa nchi hizo.