OMBI: KUOMBA KWA AJILI YA NCHI YETU NA MATAIFA MENGINE.
SIKU 21 ZA KUFUNGA NA KUOMBA – 18 JANUARI 2024
OMBI: KUOMBA KWA AJILI YA NCHI YETU NA MATAIFA MENGINE.
Ombea Ustawi wa nchi yetu na watu wake.
1 Timotheo 2:1-6, 8; 2 Nya 7:14, Wafilipi 4:6
- Toba kwa ajili ya nchi yetu na watu wake. 1 Wafalme 8:36, Yakobo 5:16
– Omba toba kwa ajili ya Kijiji/mji/jiji unakotoka, ombea watu wamgeukie Mungu na kuachana na miungu yao.
– Omba Mungu akaponye Kijiji chenu, mji wenu au jiji lenu kutokana na majanga mbalimbali (Ukame, Mafuriko, Nzige, Magonjwa, Umaskini, Ulevi n.k)
– Simama kinyume na mamlaka katika ulimwengu wa roho. Waefeso 6:12-13, 18 - Ombea Mioyo ya viongozi wa Serikali na Wanasiasa wa nchi yetu.
Mithali 21:1, Wafilipi 4:6, Mithali 21: 5
– Mioyo yao iongozwe na Bwana katika kuongoza watu. Yeremia 8:6
– Omba viongozi wakasimame katika uadilifu na kutenda haki. (Bunge na Mahakama)
– Omba tuishi Maisha ya Amani na upendo kama watanzania na wageni wanaoishi Tanzania.
– Ombea taasisi mbalimbali za serikali (Taasisi za Afya, Taasisi za Elimu, Ulinzi na Usalama n.k) - Omba kwa ajili ya Uchumi wa taifa letu na shughuli za kiuchumi.
Yeremia 27:6, Yeremia 43:10
– Ombea watu wanaotengeneza sera na sheria za uchumi kwa ajili ya kukuza na kuendeleza uchumi wa taifa hili. Isaiah 44:28, Isaiah 45:1
– Omba kwamba Mungu akafanikishe na kustawisha uchumi wetu. Kumb 28:12
– Omba baraka za Mungu juu ya Taifa letu. Zaburi 90:16-17 - Ombea Ulinzi na Usalama wa taifa la Tanzania.
– Omba Mungu alinde taifa letu. Zaburi 127:1-2
– Ombea wanajeshi wetu na familia zao.
5. Omba kwa ajili ya Mataifa Mengine.
– Omba kwa Ajili ya Mataifa ya Afrika Mashariki, SADC nk
– Omba kwa ajili ya nchi ambazo tuna mahusiano nayo kidiplomasia na Kibiashara.
– Ombea nchi ambazo ziko kwenye machafuko na mizozo.