Maombi ya siku 21, Wiki ya Tatu
Siku ya 18, Tarehe 26 January 2023.
Ombi Kuu: VIONGOZI WA SERIKALI NA VYAMA.
1. Ombea mihimili mikuu mitatu; Bunge (Kutunga Sheria), Mahakama (Kutafsiri Sheria) na Serikali (Kutekeleza Sheria) Zaburi 22:28, 1Timotheo 2:1-4.
♦ Ombea kila muhimili Mungu awape Hekima na Ufahamu katika kazi yao na kusimamia haki
♦ Ombea kila Kiongozi Mkuu wa muhimili kadiri Roho Mtakatifu atakavyokuongoza.
2. Ombea viongozi wote watumie nafasi zao kutoa haki ili amani itawale Tanzania tuishi maisha ya mshikamano na utulivu. Waefeso 6:12. Mithali 14:34. Warumi 13:1-7.
♦ Ombea Viongozi wa serikali kuanzia ngazi ya juu hadi chini.
♦ Ombea Ulinzi wa Mungu kwa kila kiongozi.
3. Ombea viongozi wote wa vyama vyote vya kisiasa. Watoe ushauri sahihi kwa serikali. Mithali 11:14
♦ Ombea Amani katika kazi zao za Kisiasa
♦ Tukatae roho za machafuko na uvunjifu wa amani.
4. Omba – Mungu atupe viongozi waadilifu. Danieli 2:21. Zaburi 33:10.
♦ Uadilifu kwa viongozi wote wanaoteuliwa na mamlaka husika.
♦ Uadilifu kwa kila mwenye dhamana ya uongozi.