UMEZALIWA KULETA MADALIKO
Mtendo ya Mitume 17:6
Paul na Mitume waliupindua ulimwengu. Walibadilisha mifumo yote uloyokuwa inapingana na injili.
na walipowakosa, wakamkokota Yasoni na baadhi ya ndugu mbele ya wakubwa wa mji, wakipiga kelele, wakisema, Watu hawa walioupindua ulimwengu wamefika huku nako,
MATENDO 17:1-6
Matendo 17:1-6 Wakiisha kupita kati ya Amfipoli na Apolonia wakafika Thesalonike, ambapo palikuwa na sinagogi la Wayahudi.
Act 17:2 Na Paulo, kama ilivyokuwa desturi yake, akaingia mle walimo, akahojiana nao kwa maneno ya maandiko sabato tatu,
Act 17:3 akiyafunua na kuwaeleza ya kwamba ilimpasa Kristo kuteswa, na kufufuka katika wafu; na ya kwamba, Yesu huyu ninayewapasha ninyi habari zake ndiye Kristo.
Act 17:4 Wengine miongoni mwao wakaamini, wakashikamana na Paulo na Sila; na Wayunani waliomcha Mungu, wengi sana, na wanawake wenye cheo si wachache.
Act 17:5 Na Wayahudi wakaona wivu, wakajitwalia watu kadha wa kadha katika watu ovyo wasio na sifa njema, nao wakakutanisha mkutano, wakafanya ghasia mjini, wakawaendea watu wa nyumba ya Yasoni, wakataka kuwapeleka mbele ya watu wa mji;
Act 17:6 na walipowakosa, wakamkokota Yasoni na baadhi ya ndugu mbele ya wakubwa wa mji, wakipiga kelele, wakisema, Watu hawa walioupindua ulimwengu wamefika huku nako,
MABADILIKO NA MAPINDUZI LAZIMA YANZE NA WEWE.
Kabla Paul na mitume wengine kupindua ulimwengu, walipinduliwa/ walibadilishwa kwaza, kimwili Kiroho, na Kifikra.
Ujume wa leo unalenga kukubadilisha wewe na njisi ya kubadilisha ulimwengu.
William Harry Mcraven ( 1955) askari mstaafu wa cheo cha juu katika jeshi la marekani. Aliongoza mapambano dhidi ya ugaidi duniani pia alikuwa mshauri wa G. Bushi kwenye maswala ya Kijeshi.
Alisema hivi:
IF YOU WANNA CHANGE THE WORLD, START OFF BY MAKING YOUR BED
Walioubadisha uliwengu walibadilishwa wao Kwanza kiroho, Kifikira na Kimwili na waliambiwa waanzie yerusalemu.
Madiliko yanaanza na wewe. Kama haujeheshimu watu hawatakuheshimu.
WALIOPINDUA ULIMWENGU WALIKUWA NAMBO YAFUATAYO
- MAONO- Mathayo 28: 19-20
19 Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;
Mat 28:20 na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.
- NGUVU ZA MUNGU- Matendo 1:8
- Walipewa nguvu za Roho mtakatifu
- Nguvu za Roho mtakatifu ziliwabadilisha
- WALIKUA NA UFAHAMU NA MAARIFA
- Mitume walikaa chini ya Yesu Kujifunza. Matendo 4:13
- Paul alikaa chini ya Gamaliel akujifunza agano la kale
- Na waumini walikaa chini ya mitume kujifunza
- Walibadilika mtazamo wao.
- Walikuwa watu wakawaida wakaanza kujiona na watu wakimataifa.
ILI UKUWE ONGEZA MAARIFA
Mithali 23:7
Maana aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo. Akuambia, Haya, kula, kunywa; Lakini moyo wake hauwi pamoja nawe.
- WALIKUWA NA BIDII
- Walijitoa kwa Mungu kikamilifu hata kwa tayari kufa.
- Bidii ya kazi- Kuhubiri, maombi
- Bidii ya kazi ya mikono. Paul alisha mahema.
- Walisafiri usiku na mchana katika mazingira magumu
Wakolosai 3:23-24
23 Lo lote mfanyalo, lifanyeni kwa moyo, kama kwa Bwana, wala si kwa wanadamu,
24 mkijua ya kuwa mtapokea kwa Bwana ujira wa urithi. Mnamtumikia Bwana Kristo.
MIFANO YA VIJANA WALIOBADILISHA ULIMWENGU WAO.
YUSUFU- MWANZO SURA YA 39-41
Joseph and Potiphar’s Wife
Gen 39:1 Basi Yusufu akaletwa mpaka Misri naye Potifa, akida wa Farao, mkuu wa askari, mtu wa Misri, akamnunua mkononi mwa hao Waishmaeli waliomleta huko.
Gen 39:2 Bwana akawa pamoja na Yusufu, naye akasitawi; naye alikuwa katika nyumba ya bwana wake, yule Mmisri.
Gen 39:3 Bwana wake akaona ya kwamba Bwana yu pamoja naye, na ya kuwa Bwana anafanikisha mambo yote mkononi mwake.
Gen 39:4 Yusufu akaona neema machoni pake, akamtumikia. Naye akamweka awe msimamizi juu ya nyumba yake, na yote yaliyomo akayaweka mkononi mwake.
Gen 39:5 Ikawa tokea wakati alipomweka awe msimamizi juu ya nyumba yake, na vyote vilivyomo, Bwana akabariki nyumba ya yule Mmisri kwa ajili ya Yusufu. Mbaraka wa Bwana ukawa juu ya vyote alivyokuwa navyo katika nyumba, na katika shamba.
Gen 39:6 Akayaacha yote aliyokuwa nayo mkononi mwa Yusufu; wala hakujua habari za kitu cho chote chake, ila hicho chakula alichokula tu.
Gen 39:7 Ikawa baada ya mambo hayo, mke wa bwana wake akamtamani Yusufu, akamwambia, Lala nami.
Gen 39:8 Lakini akakataa, akamwambia mke wa bwana wake, Tazama, bwana wangu hajui kitu kilichowekwa kwangu nyumbani, na vyote alivyo navyo amevitia mkononi mwangu.
Gen 39:9 Hakuna mkuu katika nyumba hii kuliko mimi, wala hakunizuilia kitu cho chote ila wewe, kwa kuwa wewe u mkewe. Nifanyeje ubaya huu mkubwa nikamkose Mungu?
Gen 39:10 Akawa akizidi kusema na Yusufu siku baada ya siku, lakini hakumsikia alale naye, wala aongee naye.
Gen 39:11 Ikawa, siku moja, akaingia nyumbani atende kazi yake, wala hapakuwa na mtu katika watu wa nyumbani humo ndani;
Gen 39:12 huyo mwanamke akamshika nguo zake, akisema, Lala nami. Yusufu akaiacha nguo yake mkononi mwake, akakimbia, akatoka nje.
Gen 39:13 Ikawa alipoona ya kwamba amemwachilia nguo yake mkononi mwake, naye amekimbia nje,
Gen 39:14 akawaita watu wa nyumbani mwake, akasema nao, akinena, Angalieni, ametuletea mtu Mwebrania atufanyie dhihaka. Ameingia kwangu, ili alale nami, nikalia kwa sauti kuu.
Gen 39:15 Ikawa, aliposikia ya kuwa nimepaza sauti yangu na kulia, aliiacha nguo yake kwangu, akakimbia, akatoka nje.
Gen 39:16 Basi akaiweka ile nguo kwake hata bwana wake aje nyumbani.
Gen 39:17 Naye akamwambia kama maneno hayo, akisema, Yule mtumwa Mwebrania uliyemleta kwetu, aliingia kwangu anidhihaki.
Gen 39:18 Ikawa nilipopaza sauti yangu, nikalia, akaacha nguo yake kwangu akakimbia nje.
Gen 39:19 Ikawa bwana wake aliposikia maneno ya mkewe aliyomwambia, akisema, Mtumwa wako amenitendea mambo kama haya, hasira yake ikawaka.
Gen 39:20 Bwana wake akamtwaa Yusufu, akamtia gerezani, mahali walipofungwa wafungwa wa mfalme, naye akawamo humo gerezani.
Gen 39:21 Lakini Bwana akawa pamoja na Yusufu, akamfadhili, akampa kibali machoni pa mkuu wa gereza.
Gen 39:22 Mkuu wa gereza akawatia mkononi mwa Yusufu watu wote waliofungwa, waliomo gerezani; na yote yaliyofanyika humo ndiye aliyeyafanya.
Gen 39:23 Wala mkuu wa gereza hakuangalia neno lililoko mkononi mwa Yusufu; kwa kuwa Bwana alikuwa pamoja naye. Bwana akayafanikisha yote aliyoyafanya.
- ALIKUWA NA MAONO. Mwanzo 37:5-10
- Alijua kusudi la maisha yake
- Hakubadilisha utambilisho wako
- Alitunza mahusiano yake na Mungu, alikataa kutenda dhambi
- Alikuwa mwanifu kwa Mungu
Pro 29:18 Pasipo maono, watu huacha kujizuia; Bali ana heri mtu yule aishikaye sheria.
- ALIANDALIWA KUTIMIZA MAONO- ( Discipleship)
- Alikaa chini ya Potifa, akatumika
- Kwenye jela alikwa kiongozi
- Alikuwa mfuasi kabla hajawa kiongozi
- Unahitaji kukaa chini ya watu ujifunze, soma Zaidi
3. ALIKUWA NA BIDII NA KUJITUMA
- Kila alichokifanya kilifanikiwa
- Alipewa nafasi ya kuwa kiongozi wa wafanyalaki japo alikuwa mtumwa
- Unapaswa kuwa mchapa kazi
- ALIKUWA NA NGUVU ZA MUNGU
Mwanzo 41:38 Farao akawaambia watumwa wake, Tupate wapi mtu kama huyu, mwenye roho ya Mungu ndani yake?
- Alikuwa na roho wa Mungu ndani yake
- Alimfunua Mungu katikati ya watu wasio mjua Mungu kwa kutatua matatizo ya ki uchumi ya Msiri.
- Alitunza mahusiono yake na Mungu
- Alikuwa muombaji
- Alikuwa mwaminifu
KIJANA DAUDI 1 Samuel 16
Daudi alikuwa mototo wa mwisho wa Yese kati ya watoto 8. Alipakwa mafuta kua mfalme akiwa na miak 15 na akanza kutawala Israeli akiwa na miaka 30.
Alibadilisha historia ya taifa la Israel
- ALIKUWA NA MAONO YA KUWA MFALME WA ISRAEL
1Sa 16:12 Basi akatuma mtu, naye akamleta kwao. Naye alikuwa mwekundu, mwenye macho mazuri, na umbo lake lilikuwa la kupendeza. Bwana akasema, Ondoka, umtie mafuta; maana huyu ndiye.
1Sa 16:13 Ndipo Samweli akaitwaa pembe yenye mafuta, akamtia mafuta kati ya ndugu zake; na roho ya Bwana ikamjilia Daudi kwa nguvu tangu siku ile. Basi Samweli akaondoka, akaenda zake Rama.
- ALIANDALIWA KUWA KIONGOZI
- Alikaa ikulu akipiga mziki kuondoa roho mbaya kwa sauli
- Alijufunza mambo ya kijeshi na uongozi
- Akapitia kwenye moto
- Akaangoza watu wachache na baadae taifa
David in Saul’s Service
1Sa 16:14 Basi, roho ya Bwana ilikuwa imemwacha Sauli, na roho mbaya kutoka kwa Bwana ikamsumbua.
1Sa 16:15 Nao watumishi wa Sauli wakamwambia, Angalia, sasa roho mbaya kutoka kwa Mungu inakusumbua.
1Sa 16:16 Basi bwana wetu na atuamuru sisi watumishi wake waliopo hapa mbele yako watafute mtu aliye stadi wa kupiga kinubi; basi itakuwa, roho ile mbaya kutoka kwa Mungu itakapokujilia, yeye atapiga kinubi kwa mkono wake, nawe utapona.
1Sa 16:17 Basi Sauli akawaambia, Vema, nitafutieni mtu aliye stadi wa kupiga kinubi, mkaniletee.
1Sa 16:18 Ndipo akajibu mmoja wa watumishi wake akasema, Tazama, nimemwona mwana mmoja wa Yese, Mbethlehemi, aliye stadi wa kupiga kinubi, tena ni mtu shujaa, hodari wa vita, anenaye kwa busara, mtu mzuri, ambaye Bwana yu pamoja naye.
1Sa 16:19 Basi Sauli akampelekea Yese wajumbe, akasema, Nipelekee Daudi mwanao, aliye pamoja na kondoo.
1Sa 16:20 Yese akatwaa punda, wa kuchukua mikate, na kiriba cha divai, na mwana-mbuzi, akampelekea Sauli kwa mkono wa Daudi mwanawe.
1Sa 16:21 Basi Daudi akamwendea Sauli, akasimama mbele yake, naye akampenda sana; naye akapata kuwa mtu wa kumchukulia silaha zake.
1Sa 16:22 Kisha Sauli akapeleka watu kwa Yese, akasema, Tafadhali, mwache Daudi asimame mbele yangu; maana ameona kibali machoni pangu.
1Sa 16:23 Ikawa, ile roho mbaya kutoka kwa Mungu ilipomjilia Sauli, ndipo Daudi akakishika kinubi, akakipiga kwa mkono wake, naye Sauli akaburudishwa, na ile roho mbaya ikamwacha.
- ALIKUWA NA BIDII
- Alichunga kondoo kwa uaminifu
- Aliendeleza kipawa chake
- Alikuwa mpganaji hodari
- ALIKUWA NA NGUVU ZA MUNGU
- Alikuwa muombaji. Kuomba ilikuwa ni maisha yake
- Hakufanya jambo lolote bila kumuuliza Mungu
- Alikipopiga muziki mapepo yalimuachia Saul
- Alimshinda Goliath kwa nguvu za Mungu
KIJANA DANIEL
DANIEL 1:1-21
Alikuwa na ni kijana kutoka kwenye familiya ya kifalme. Waisrael wakapelikwa utumwani baada Bebeli kutawala taifa la Irael. Walichaguliwa vijana wachache wakwenda kutumika kwa mfalme wa Babeli.
- MAONO YAKE
– Kumfunua Mungu katika mataifa, na kusimamia kusudi la Mungu juu ya Israel
– Alikuwa na nidhamu
– Alikuwa mwamnifu kwa Mungu
2. ALIFUNDISHWA
- Alikuwa msomi
- Alipofika Babel pia akasoma
- ALIKUWA NA BIDII
- Alifaulu sana kwenye masomo
- Bidii ya neno na kuomba
3. ALIKUWA NA NGUVU ZA MUNGU - Aliomba maratatu kwa siku
- Alikuwa na karama ya kutafsri ndoto
- Alitunza mahusiono yake na Mungu
HITIMISHO
KIJANA WEWE LAZIMA UWE NA MAONO.
- Kutumikia kusudi la Mungu
- Uwe na nithamu.
- Uwe na muelekeo.
- Weka mipaka katika maisha yako
- Tunza mahusiano yako na Mungu.
Mfano . wana michezo.
ENDELEA KUJIFUNZA.
- Kaa chini ya viongoze wako jifunze
- Uwe bora katika eneo lako
- Endeleza kipawa chako
UWE NA BIDII
- Kila unachokifanya ukifanya kwa bidii
TEMBEA KATIKA NGUVU ZA MUNGU
- Uwe na maisha ya maombi
- Tunza kibali cha Mungu katika maisha yako
Download/listen here Reborn to impact/ Umezaliwa Upya kuleta mabadiliko