Huduma ya Watoto Climb


Huduma ya Climb inajihusisha na kufundisha Neno la Mungu kwa Watoto wote wenye umri wa miaka 1-12  na vijana wadogo wenye umri wa miaka 13-19. Hili linafanyika kwa kutumia kipawa cha kufundisha ambacho Mungu amewabariki watu wake.

Mithali 22:6

“Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha hata atakapokuwa mzee”

Kufundisha watoto KUMPENDEZA Mungu katika kila jambo wanalolifanya, KUPENDANA na KUMFUATA Kristo. KUWAJENGA, kihuduma, kutumika kwa ajili ya wengine na KUENEZA Injili Ulimwenguni kote!

Madarasa yamegawanyika kwa umri katika makundi matano

  • Miaka 0-3
  • Miaka 4-6
  • Miaka 7-9
  • Miaka 10-12
  • Miaka 13-19

Walimu wameandaliwa vema, wana moyo wa kujitoa na wanfanya bidii yote kuandaa Mazingira mazuri  yakufurahisha katika kufundisha Neno la Mungu na wanawasaidia watoto,  kuelewa  vizuri maandiko.

Njia zinazotumika kufundishia ni kama;  , Majadiliano, vielelezo vya picha, Maswali na majibu, Michezo, hadithi za Biblia,ubunifu wa vitendo, Kupaka rangi picha, kutafiti, Maigizo na kuwa mbunifu wa kufanya ufundishaji wenye kufurahisha na kuchangamsha.

MATUKIO YA MWAKA

  • Shule ya Biblia (VBS)

Inafanyika mwezi wa Juni/Julai  kwa watoto wenye umri wa miaka 3-12

  • Mafunzo kwa Waalimu mwezi wa machi

MATUKIO YA MSIMU

  • Maonyesho ya Pasaka
  • Maonyesho ya Krismasi

MATUKIO YA MWEZI

  • Upendo Bible Club (UBC)

Inafanyika jumamosi ya mwanzo wa mwezi kwa Watoto wenye umri wa miaka  8-12.

MATUKIO YA WIKI

  • Shule ya Jumapili kwa Watoto wenye umri wa miaka 6-12
  • Darasa la vijana rika miaka 13-19

UINJILISTI NA USHUHUDIAJI

  • Makusanyiko ya Watoto kwa ajili ya Uinjilisti au kutoa kwa ajili ya wenye uhitaji
  • Uimbaji wa Nyimbo za Mungu wakati wa Krismasi kwenye Jiji (i.e. Mlimani City)

JINSI YA KUSHIRIKI KWENYE HUDUMA YA CLIMB

Ni rahisi!  Unaweza kushiriki kwa njia zifuatavyo

  • Kuombea huduma
  • Kusaidia kutafsili vitabu vya kujifunzia kutoka Kiingereza kwenda Kiswahili
  • Kufundisha darasani au kumsaidia mwalimu anayefundisha
  • Kutoa vitabu, midoli, zawadi za krismasi, vitafunio, pipi au vinywaji

Join the Discussion

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top