BWANA NI MTETEZI WAKO

BWANA NI MTETEZI WAKO. Isaya 54:10–17; Zaburi 23:4


Mafundisho Muhimu:

1. Upendo wa Mungu Hauna Kikomo

Isaya 54:10–12; Yeremia 31:3; Luka 15:17–20
Upendo wa Mungu hautetereki wala hauishii. Hata milima ikiondoka na vilima kutikisika, upendo Wake kwetu hudumu milele. Yuko tayari kutupokea tena hata pale tunapokuwa tumeanguka, kama baba alimkaribisha mwana mpotevu kwa shangwe.


2. Ulinzi wa Mungu Uko Juu ya Kila Hali na Kila Sila

Isaya 54:16; Zaburi 7:15–16; Danieli 6:16–23; Esta 7:9–10
Mungu ndiye mtengenezaji wa kila silaha, na hakuna chochote kinachoweza kumshinda. Hakuna njama, shimo, wala hila inayoweza kufanikiwa dhidi ya watu Wake. Yeye huwalinda waaminio Wake hata katikati ya simba au maadui wenye nguvu.


3. Ulinzi ni Urithi Wako, na Utetezi Wako Watoka kwa Mungu

Isaya 54:17; Zaburi 23:4; Zaburi 91:1–2; Danieli 3:17; Mithali 18:10
Ulinzi wa Mungu ni sehemu ya urithi wa kila mwana wa Mungu. Tuna hakikisho la kinga dhidi ya kila mashambulizi, kwa maana jina la Bwana ni ngome imara – wenye haki hukimbilia humo na kuwa salama. Hata tutakapopita katika bonde la uvuli wa mauti, hatutaogopa mabaya.

×Note: To download, click the button. If it doesn't work, right click, then click "Save Link As." Download only works if media is stored within this site. Download Video

Join the Discussion

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top

Share with