MTUMAINI BWANA NYAKATI ZOTE. ISAYA 40:28 – 31; ZABURI 62:8
- Kutumaini– kuwa na Imani, kutegemea, kuwa na uhakika juu ya mtu au jambo fulani.
- Kumtumaini Bwana – kumwamini na kumtegemea
- MUNGU NI WA MILELE NA MWENYE UWEZA WOTE
Isaya 40: 27 – 28; zaburi 90:2; 62:8
Key verses
Isaya 40:28 Je! Wewe hukujua? Hukusikia? Yeye Mungu wa milele, BWANA, Muumba miisho ya dunia, hazimii, wala hachoki; akili zake hazichunguziki.
Zaburi 90:2 …Na tangu milele hata milele ndiwe Mungu.
2. MUNGU HUWAPA NGUVU WALIOCHOKA NA WANYONGE. Isaya 40:29
Key verse Isaya40:29. Huwapa nguvu wazimiao, humwongezea nguvu yeye asiyekuwa na uwezo.
Waliochoka – nguvu zimekwisha, waliolemewa na mizigo, waliokata tamaa kwa sababu ya changamoto mbalimbali.
- Eliya – alikata tamaa na kuomba Mungu amuue. (1Fal 19:1 – 8)
- Mungu akamtia nguvu aendelee mbele.
Wanyonge/dhaifu – wasiokuwa na uwezo au nguvu.
- Gideon – alijiona dhaifu, hastahili, sio shujaa.
- Mungu akampa jina “shujaa, Hodari.”
- Mungu alimpa nguvu na ushindi.
3. NGUVU ZA MUNGU HUWEZESHA WATU WAKE KUSHINDA CHANGAMOTO
Isaya 40:30 – 31; Ayubu 19: 19 – 20; 25 – 26
Key verses. Isaya 40: 31 bali wao wamngojeao BWANA watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watakimbia, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia.
Ayubu 19:25 Lakini mimi najua ya kuwa Mteteaji wangu yu hai, Na ya kuwa hatimaye atasimama juu ya nchi.







