MUNGU AMEKUWEZESHA ILI KUTUMIKA
Neno 1 Pet 4:10
UTANGULIZI
- Petro aliwaandikia wakristo (ambao sio wayahudi) wa utawanyiko (exiled) katika mikoa 5 ya Kirumi ambayo kwa leo ni Uturuki. Aliandika kwa dhumuni la kuwakumbusha kuhusu tumaini lao, kuvumilia, utambulisho wao mpya, na mwenendo wa heshima.
- Katika mlango wanne ameongelea kumuishia Mungu (1 Pet 4:1-11) na mateso kwa kuwa Mkristo (1Pet 4:12-19)
SOMO 1: MUNGU NDIYE MTOA KARAMA
Karama ni nini?
- Karama ni uwezo wa kiungu unaotolewa bure na Roho Mtakatifu kwa mwamini.
- Karama ni zawadi ya kiroho, uwezo wa pekee, au neema inayotolewa na Mungu kwa mtu kwa ajili ya kuwatumikia na kuwajenga wengine, hasa ndani ya kanisa au jamii.
- Mungu ndiye aliyetuumba, hivyo Yeye ndiye anayejua ni uwezo, karama gani aliokupa au unayohitaji au atakayokupa.
Utajuaje kama Mungu amekupa karama?- Roho Mtakatifu ndiye atakusaidia kutambua hilo
1 Kor 2:12, Yn 16:13-14
1 Kor 2:12
Lakini sisi hatukuipokea roho ya dunia, bali Roho atokaye kwa Mungu, makusudi tupate kuyajua tuliyokirimiwa na Mungu.
1 Kor 12:4-11
“4 Basi pana tofauti za karama; bali Roho ni yeye yule. 5 Tena pana tofauti za huduma, na Bwana ni yeye yule. 6 Kisha pana tofauti za kutenda kazi, bali Mungu ni yeye yule azitendaye kazi zote katika wote. 7 Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa kufaidiana. 8 Maana mtu mmoja kwa Roho apewa neno la hekima; na mwingine neno la maarifa, apendavyo Roho yeye yule; 9 mwingine imani katika Roho yeye yule; na mwingine karama za kuponya katika Roho yule mmoja; 10 na mwingine matendo ya miujiza; na mwingine unabii; na mwingine kupambanua roho; mwingine aina za lugha; na mwingine tafsiri za lugha;11 lakini kazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja, yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye.”
SOMO 2: KARAMA NI KWAAJILI YA HUDUMA
- Dhumuni la kuumbwa na kupatinishwa kwetu na Mungu sio ili tuishi halafu tufe. Mungu tayari alipanga tokea awali kuwa tutende matendo mema.
Efe 2:10, (Tito 2:14)
Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo.
- Biblia imetupa mwongozo wa nini cha kufanya na karama tulizopokea- kuhudumiana.
1 Pet 4:10
“kila mmoja kwa kadiri alivyoipokea karama, itumieni kwa kuhudumiana; kama mawakili wema wa neema mbalimbali za Mungu.”
1 Kor 14:12 “Vivyo hivyo na ninyi, kwa kuwa mnatamani sana kuwa watu wenye karama za roho, takeni kwamba mzidi sana kuwa nazo ili kulijenga kanisa.”
- Mtu akikupa zawadi huwa anakupa kitu ambacho utatumia, kitachokusaidia/kukuhudumia. Vivyo hivyo Mungu ametupa karama ili tuhudumiane.
1 Kor 12:7-10
“7 Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa kufaidiana. 8 Maana mtu mmoja kwa Roho apewa neno la hekima; na mwingine neno la maarifa, apendavyo Roho yeye yule; 9 mwingine imani katika Roho yeye yule; na mwingine karama za kuponya katika Roho yule mmoja; 10 na mwingine matendo ya miujiza; na mwingine unabii; na mwingine kupambanua roho; mwingine aina za lugha; na mwingine tafsiri za lugha;
- Mbinguni hamna uhitaji wa neno la hekima, maarifa, uponyaji etc(1 Kor 12:8-10) kwahiyo karama hizi ni za kutumia hapa duniani.
Rum 12:4-8 SUV
“4 Kwa kuwa kama vile katika mwili mmoja tuna viungo vingi, wala viungo vyote havitendi kazi moja; 5 Vivyo hivyo na sisi tulio wengi tu mwili mmoja katika Kristo, na viungo, kila mmoja kwa mwenzake. 6 Basi kwa kuwa tuna karama zilizo mbalimbali, kwa Kadiri ya neema mliyopewa; ikiwa unabii, tutoe unabii kwa Kadiri ya imani; 7 ikiwa huduma, tuwemo katika huduma yetu; mwenye kufundisha, katika kufundisha kwake; 8 mwenye kuonya, katika kuonya kwake; mwenye kukirimu, kwa moyo mweupe; mwenye kusimamia kwa bidii mwenye kurehemu, kwa furaha.”
- Mungu hakumbariki Abramu ili awe na baraka ila alimalizia kwa kumwambia ili awe baraka kwa wengine.
Mwa 12:1-2 BWANA akamwambia Abramu, Toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonyesha; nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka.
SOMO 3: KUTUMIKA NI UWAKILI MWEMA WA NEEMA YA MUNGU
1 Pet 4:10, Luka 12:42
“Bwana akasema, Ni nani, basi, aliye wakili mwaminifu, mwenye busara, ambaye bwana wake atamweka juu ya utumishi wake wote, awape watu posho kwa wakati wake?”
- Mungu amekupa neema yake ili uitumie. Unaitumiaje?- ni kwa kutumika.
- Kutokutumika ni kupokea neema ya Mungu bure.
1 Kor 15:10
“Lakini kwa neema ya Mungu nimekuwa hivi nilivyo; na neema yake iliyo kwangu ilikuwa si bure, bali nalizidi sana kufanya kazi kupita wao wote; wala si mimi, bali ni neema ya Mungu pamoja nami”
2 Kor 6:1
“Nasi tukitenda kazi pamoja naye twawasihi msiipokee neema ya Mungu bure”
- Yesu pia alikuja kutumika (Marko 10:45 SUV “Kwa maana Mwana wa Adamu naye hakuja kutumikiwa, bali kutumika, na kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi)
- Tukiongelea swala la uwakili huwa tunarudi kwenye mfano ulioandikwa katika Mat 25: 14-30
- Aliepewa talanta 5 na 2 waliambiwa (Mat 25:21&23 BHN) “Vema, mtumishi mwema na mwaminifu. Umekuwa mwaminifu katika mambo madogo, nitakukabidhi makubwa”
- Aliepewa talanta 1 aliambiwa (Mat 25:26,28,30 BHN)“ 26 Wewe ni mtumishi mwovu na mvivu! …… 28 Basi, mnyanganyeni hiyo fedha mkampe yule mwenye talanta kumi……. 30 Na kuhusu huyu mtumishi asiye na faida, mtupeni nje gizani!”
- Efe 2:10 inasema Mungu alituumba ndani ya Kristo Yesu ili tufanye matendo mema.
HITIMISHO
1 Pet 4:1-6






