TUSIENDE HUKO BALI TWENDE KWA YESU. YOHANA 6: 55 -70
- Neno “HUKO” – ni kumaanisha – “mahali pale au sehemu ile”.
- Lakini kwa ajili ya ujumbe wetu leo twaweza maanisha:
- Mahali fulani, watu fulani, vitu fulani (maarufu)
- Kufuata watu wenye ushawishi mkubwa, watu maarufu
- Kukimbilia (focus) watumishi feki wa injili, baba wa kiroho
Yesu alipowambia Wayahudi kuwa, “Yeye ni chakula kilichoshuka kutoka mbunguni” – wengi wao waliaanza kunung’unika na kuanza kuondoka
- Yesu anawauliza Mitume 12 kama na wao wanataka kuondoka
- Mtume Petro akamjibu Yesu akisema – Bwana! Twende kwa nani?
- Natumaini nasi leo tunasema kama Petro na hatutaondoka kwa Yesu
Sababu za kutufanya twende kwa Yesu:
I. YESU ANAYO MANENO YA UZIMA WA MILELE. Yohana 6: 68, Mathayo 8:8,13, Mathayo 24:35
· Sote tunakumbuka jinsi Yesu alivyotoa maneno ya uzima kwa wale waliokuwa katika matatizo – mwanamke Msamaria, mwanamke mwenye damu, kipofu, kuwalisha watu wenye njaa, Lazaro aliyekuwa amekufa, hata mtumishi wa Jemadari aliyekuwa mgonjwa – Mathayo 8:8,13
· Maneno ya uzima yaliendelea kutoka kwa Yesu, yakiponya na kubariki wenye uhitaji. Maneno Yake bado yamejaa uzima, urejesho, amani, huruma, upendo, na kujali.
· Ni maneno ya Mungu yasiyopitwa na wakati; mbingu na dunia zitapita, lakini maneno Yake hayatapita kamwe – Mathayo 24:35
II. YESU ANAO UPAKO MAALUMU KWA AJILI YAKO. Yohana 6: 69, Luka 4:18, Zaburi 23:1
Siku hizi waumini wanazunguka huku na kule wakitafuta upako.
- Fahamu kwamba Yesu Kristo anao upako maalum kwa ajili yako – Luka 4:18
- Mtume Petro alikiri ni kwa nini hawakuweza kuondoka kwa Yesu – Yesu ni Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.
- Jina “Kristo” lina maana ya kipekee (kwa Wayahudi na kwetu sote) – “Aliyepakwa mafuta” au “Masihi.”
- Kristo anao upako wa kutumikia, kuweka huru, na kutangaza neema ya Bwana kwa watu wote.
- Kristo ndiye Masihi – Mfalme wa wafalme na mwenye uwezo wa kuwakomboa watu wake.
Ninapomaliza, tukumbuke kwamba Yesu Kristo ni Mchungaji wetu, nasi hatutapungukiwa na kitu chochote tukiwa pamoja Naye – Zaburi 23:1.
Na kwa sababu hiyo, tusikimbilie huku na kule bali tukae na Yesu daima, hata katika hali ngumu.
Na tuazimie kumtazama Yesu pekee, wala si kitu kingine. Tuweze kusema kwa fahari kama Petro: “Bwana, tuende kwa nani?” – hata kama tutawaona wengine au rafiki zetu wakimwacha Yesu.






