MATHAYO 11:28-30
- Yesu aliposema twende kwake ili atupumzishe na mizigo, ni wazi kwamba alijua watu wengi wamebeba mizigo mizito tena inayowalemea
- Mizigo hii ya shida na mateso imewafanya watu wengi hata kukata tamaa na kuvunjika moyo katika maisha yao
- Yesu Kristo kwa kuzijua shida na mateso watu wanayopitia anatoa wito uliojaa faraja na huruma kwamba tunapolemewa, basi tukimbilie kwake
- Huu ni wito uliojaa pumuziko na tumain la kweli katika imani zetu kwake
I# YESU ATATUPATIA PUMZIKO – Mathayo 11: 28-30
- Ikumbukwe kuwa kwa Yesu kunapatikana pumziko la kweli – lenye raha
- Mara nyingi mtu aliyechoshwa na kulemewa na mizigo huitaji pumziko
- Pumziko linampa mtu nguvu na hali mpya ya kuendelea mbele tena
- Pumziko laweza kumpa mtu mawazo na mbinu mpya ili kuendelea mbele
- Yesu ameahidi kutupa pumziko wale wote tuliolemewa na mizigo mingi
- Hii yaweza kuwa mizigo ya njaa, magonjwa, umaskini, vita na mapigano (kimwili, kiroho, familia/ukoo, mahusiano, na hata katika utumishi)
- Ili Yesu atupumzishe na hayo yote, lazima tuchukua hatua ya kumwendea
- Tumwamini, tumtegemee, tumuombe kama yeye mwenyewe alivyofanya mbele za Baba yake – Luka 6:12, nasi tuendelee kuomba – Mathayo 7:7-8
II# YESU ATATUONGEZEA IMANI – Luka 17:1-5
- Mtu anapolemewa na mizigo (shida na mateso) kama tulivyotaja hapo juu – njaa, magonjwa, umaskini na majaribu mengine mengi – imani yake wakati mwigine yaweza kushuka ama kuyumba
- Ndio maana Yesu anasema tujipe moyo –Yeye ameushinda ulimwengu hivyo nasi tutashinda kwa uweza wake – Yohana 16:33
- Tukimwendea Yesu hakika atatuongezea imani ili tushinde majaribu – Marko 9:14-29 – (mzazi wa mtoto), Mathayo 17:19-21– (wanafunzi wake)
MWISHO, Mathayo 8:23-27 – kumwendea Yesu tunapolemewa na mizigo ni hatua ambayo hata wanafunzi wa Yesu mwenyewe waliichukua. Hivyo, twendeni kwa Yesu ili atupumzishe na mizigo ya dunia hii na kutuongezea imani.






