WEWE NI WAKILI WA SIRI ZA MUNGU.
1Wakorintho 4:1 – 2; Warumi 14:12
Maneno muhimu: (Bible Dictionary)
- Mtumishi – Gk hyperetes mtu anaefanya kazi chini ya mamlaka ya mwingine na kutekeleza majukumu aliyopewa na mwenye mamlaka.
- wakili – Gk kutoka “oiko” nyumba and “nomos” kusimamia.
- wakili – “oikonomos” aliyepewa dhamana kusimamia mali au rasilimali ambazo si zake, bali amekabidhiwa na bwana wake.
- siri – Gk Mysterion – jambo au kitu kilichofichwa au jambo ambalo halijajuikana kwa wengine mpaka lifunuliwe.
- Sisi ni watumishi na mawakili wa siri za Mungu (1Cor.4:1)
- TAMBUA KILE MUNGU ALICHOKUKABIDHI 1Wakorintho 4:1; Waefeso 3:7 – 8; 1Petro 4:10
- Paulo alitambua alichokabidhiwa – Injili ya Kristo kwa mataifa.
Ephesians 3:7 – 8
7 Injili ambayo nilifanywa mhudumu wake, kwa kadri ya kpawa cha neema ya Mungu niliyopewa …kuwahubiri mataifa…
- Inakupasa kutambua huduma yako.
2. UWE MWAMINIFU KATIKA KILE MUNGU ALICHOKUKABIDHI 1Wakorintho 4:2; Warumi 12:6 – 8
- Hapo tena ianayohitajika katika wakili, ndiyo mtu aonekane mwaminifu(1Kor. 4:2).
Mifano ya watu waliofanya kwa uaminifu:
- Musa – uongozi na alifanya kwa uaminifu Kutoka 3:10 – 12
- Yusufu – utawala na alifanya kwa uaminifu na uadilifu Mwanzo 41:39 – 41.
- Ruth – Kumuangalia mjane na alifanya kwa moyo Ruth 2:11 – 17.
- Paul – Injili na alifanya kwa uaminifu mpaka kufa Matendo 20:24.
3. UTATOA HESABU YA KILE MUNGU ALICHOKUKABIDHI
Warumi 14: 12; Luka 12:47 – 48; Matthayo 25:21
- Utatoa hesabu ya maisha yako.
- Utatoa hesabu ya watoto Mungu aliokukabidhi.
- Utatoa hesabu ya karama na vipawa Mungu alivyokupa.
- Utatoa hesabu ya muda, mali, nafasi yako, huduma nk.
Conclusion
- Kila mtu na awe mwaminifu kwa kile alichopewa.
- Bwana wetu, Yesu Kristo aweze kuseme VEMA MTUMWA MWEMA!!!
- Na kama hujawa mtumwa mwema, omba Mungu akusaidie.
×Note: To download, click the button. If it doesn't work, right click, then click "Save Link As." Download only works if media is stored within this site. Download Video






