YALIYOKUTESA 2024 HAYATAKUTESA 2025

YALIYOKUTESA 2024 HAYATAKUTESA 2025

KUTOKA 14:10-14

  • Moja ya tukio lenye mguso kuhusu wana wa Israeli katika safari ya kutoka utumwani wakielekea inchi ya ahadi – Kanaani ni pale walipovuka the Red Sea. 
  • Jambo hili kibinadamu ilikuwa haliwezekani bali kwa uweza na nguvu za Mungu Bahari iligawanyika wana wa Israeli wakapita 
  • Hayo yote yalifanyika ili Mungu ajitwalie utukufu na kuzidi kuthibitisha kuwa yeye ndie Mungu mkuu na muumbaji wa vitu vyote – Vs. 4

Briefing on the Israelites Story:

  • Sote tunajua wana wa Israeli walichukuliwa utumwani nchini Misri – (400 years)
  • Ulipofika muda wao kutoka utumwani ili kwenda inchi ya ahadi -Kanaani
  • Farao hakuwa tayari kuwaachia waende bali kuendelea kuwatumikisha 
  • Baada ya mapigo mengi kutoka kwa Mungu – Farao aliwaacha waende    
  • Farao anaona kama amekosea kuwaacha Waisraeli waondoke – Vs.5
  • Hivyo, anafanya maamuzi ya kuwafuata awarejeshe tena katika utumwa 
  • Anafanya hivyo bila kujua kwamba MUNGU yuko pamoja na Waisraeli 
  • Na hapo ndipo Farao na jeshi lake lote wanaangamizwa na Mungu  
  • Mungu anatangaza kuwaangamiza Wamisri – adui wa wana wa Israeli na kwamba hawataonekana tena – Na, ndivyo ilivyokuwa.

Lessons to take home:

#1.       Naomba usiku huu nikutangazie kuwa YALIYOKUTESA 2024 HAYATAKUTESA 2025

  • Kwa sababu Bwana Mwenyewe atakupigania, nawe utanyamaza kimya
  • Yakupasa kuendelea mbele bila kujali mazingira – (Bahari kubwa)
  • Amini kuwa Bwana atakupitisha mahali pakavu katikati ya Bahari
  • Mungu atakutendee hivyo ili yeye mwenyewe ajitwalie utukufu na heshima
  • 2025 utakuwa ni mwaka wa kujua kuwa Mungu yuko upande wako
  • Mungu atanyosha mkono wake kukutetea, na utawaona adua zako wakiteketekea

#2.       ENDELEA KUWEKA TUMAINI LAKO KWA MUNGU 

  • Kuendelea kumtumaini Mungu ni kuendelea kumwani Mungu. 
  • Kumtumaini Mungu kunatupa nguvu ya kupita na kuvuka jangwani.
  • Kumtumaini Mungu kunatufanya tusife jangwani hata kama kuna mauti
  • Tumaini linatupa kupita katika bonde la uvuli wa mauti bila hofu – Zaburi 23:4
  • Kutumaini katika Mungu kunatuondolea hofu na kutupa kusimama imara.
  • Kuweka tumaini kwa Mungu hutuletea wokovu na ushindi zaidi ya adui yeyote. 
  • Kuweka tumaini kwa Mungu kunatupa kufikia na kuona mwisho wa safari.
  • Kukosa tumaini na imani kwa Mungu kwaweza kukusababishia kufa ama kukaa muda mrefu jangwani – (Israeli 40 years) bila kuvuka. 

Nimalize kwa kukutia moyo kuwa, 2025 endelea mbele ukimtumaini Mungu kwani yeye ndie fungu lako – Maombolezo 3:24

Yeye mwenyewe atafanya njia ya kutokea hata kama umezungukwa na Bahari kubwa.
Anza mwaka kwa imani kubwa na matumaini mengi kuwa yaliyokutesa 2024 hayatakutesa 2025.           

×Note: To download, click the button. If it doesn't work, right click, then click "Save Link As." Download only works if media is stored within this site. Download Video

Join the Discussion

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top