1. KAA MBELE ZA MUNGU KATIKA IBADA NA TOBA
a) Mwabudu, Msifu na kumshukuru. (Ufunuo 4: 8-11 na Zaburi 89: 1-18).
b) Weka moyo wako na dhamiri yako sawa kwa njia ya kupokea msamaha wa dhambi. (2 Wakorintho 5: 17-21 na Waefeso 1).
2. KUBALIANA NA ROHO MTAKATIFU
Kujiombea /idara zote / Watumishi walioalikwa. Chukua muda kutambua kila kitu kizuri kilicho ndani yako katika Kristo Yesu. Filemoni 1: 6.
Amini na umshukuru Mungu:
• Ambaye hufanya kazi ndani yako kutaka na kutenda kwako ili kulitimiza kusudi lake jema. Wafilipi 2:13
• Kwamba umeumbwa katika Kristo kufanya matendo mema, ambayo Mungu aliyatengeneza tangu mwanzo ili tuenende nayo. Waefeso 2:10
• Kwamba ni Mungu mwenyewe anayefanya kazi ndani yako kama alivyofanya katika Kristo. 2 Wakorintho 5: 20-21.
• Kwamba amekutia mafuta na unajua mambo yote. (1Yohana 2: 20 & 27).
• Kwamba amekujaza kipimo cha imani kwa ajili ya huduma. Warumi 12: 3-8
• Kwa sababu unaamini utafanya kazi za Mungu. Yohana 6: 28-29.
• Kwamba kila atakayehudumu atakuwa na umoja na nia moja. (Yohana 17: 21-23 na Wafilipi 2: 1-2).
• Kwa mwongozo wa Roho Mtakatifu katika kweli yote. Yohana 16: 12-15
3. OMBEA IBADA NZIMA KWA MUJIBU WA NENO:
• Uwepo wa Mungu ili kutimiza kusudi lake kwa watu wake.
☆ 1 Wafalme 8: 10-11, Matendo 2: 4
☆ Marko 16: 17-18
☆ 2 Wakorintho 3:17
☆ Yohana 16: 23-24.
• Neno, Mnenaji wa Neno na Mtafsiri.
☆ Isaya 50: 4-5
☆ Waefeso 1: 9-10
• Mahudhurio.
Tangaza kile unachotaka kuona juu ya mahudhurio katika ubora na wingi.
4. SHUKRANI KWA MUNGU
Mshukuru Mungu kwa kutimiza ahadi zake kulingana na Zaburi 136. Imba kama Daudi alivyoimba !!!