UJUMBE: YATUPASA KUWA NA USHIRIKA NA WENGINE
KIFUNGU: MATENDO 2: 42
USHIRIKA – ni hali ya kushirikiana kwa ajili ya faida ya pande zote.
- Ushirika ni kitu ambacho kinahitajika kwa wanadamu,wanyama, ndege …
- Mwanadamu ni kiumbe kinachohitaji ushirika – ndio maana Mungu ilibidi amuumbe Hawa ili kuondoa upweke wa Adamu – MWANZO 2:18
- Hivyo kutoa ushirika sahihi kwa mwenza ni kati ya mambo ya msingi sana kwa mwanandoa yeyote yule.
- Tena kwa mwanadamu – jambo la ushirika ni hitaji la kisaikologia na kijamii
- Pia ndani ya kanisa la mahali, ushirika unabaki kuwa suala nyeti sana linalowafanya waumini kuwa hai, wawajibika, na kitu kimoja
- Hivyo kulingana na uelewa huo, kuhimiza suala la ushirika inabakia kuwa kazi ya muhimu sana ndani ya kanisa na katika vikundi vidogo vidogo.
- Katika mazingira ya kikanisa, ushirika unaweza kuonekana katika kundi kubwa kama vile ibaada ya Jumapili, au katika kundi dogo kama vile kwenye cell, ibaada za wamama, wababa, au vijana, kwenye kwaya, Bible study.
- Makundi yote haya na mengine mengi yanawasaidia waumini kupata ushirika
- Hivyo basi, ni vyema sana kila muumini ndani ya kanisa kuhakikisha yuko kwenye kikundi kimoja wapo au vikundi zaidi ya kimoja
- Na hii ifanyike huku tukijua kuwa ushirika unaongeza ushirikianao na urafiki
- Na pia ushirika unawapa nafasi waumini wachanga kujifunza kwa waumini walikomaa katika imani na kutuimarisha kwa pamoja.
Ushirika ni hali ya kushirikiana kwa ajili ya faida ya pande zote.
Ushirika ni kitu ambacho kinahitajika kwa wanadamu,wanyama, ndege
Mwanadamu ni kiumbe kinachohitaji ushirika
Ndio maana Mungu ilibidi amuumbe Hawa ili kuondoa upweke wa Adamu
[MWANZO 2:18] BWANA Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye.
MAMBO YA KUFANYA NDANI YA USHIRIKA
- KUFUNDISHA NENO LA MUNGU
YESU akajibu, “Imeandikwa, Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu” – MATHAYO 4:4 Neno lako ni taa ya miguu yangu, Na mwanga wa njia zangu – ZAB. 119:105Ushirika unatupa nafasi ya kujadili neno la Mungu pamoja na kujenga uwezo wa kufundisha na kuhubiri juu ya Yesu Kristo – MATENDO 5:42 Kufundisha na kujifunza neno la Mungu kunatuwezesha kumjua Mungu zaidi MATHAYO 4:4 Yesu akamjibu, “Imeandikwa: ‘Mtu haishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno asemalo Mungu.’”, ZAB 119:105 Mwachie Mwenyezi-Mungu mzigo wako, naye atakutegemeza; kamwe hamwachi mwadilifu ashindwe, MATENDO 5:42 Wakaendelea kila siku kufundisha na kuhubiri Habari Njema ya Kristo hekaluni na nyumbani kwa watu. - KUOMBA PAMOJA
Kuomba pamoja kunatuimarisha kiroho na kukuza imani zetu katika Mungu. Kunatupa nafasi ya kuombeana na kuomba kwa ajili ya shida na mahitaji yetu – WAGALATIA 6:2 – “Mchukuliane mizigo …”Pia inatuwezesha kuombea mahitaji ya kanisa na huduma zake zoteKunamfanya Mungu aje na kukaa katikati yetu na kujibu maombi yetu – MATHAYO. 18:19-20 “… Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao”.
WAGALATIA 6:2 Chukulianeni mizigo yenu; na kwa njia hiyo mtaweza kutimiza sheria ya Kristo, MATHAYO. 18:19-20 Tena nawaambieni, wawili miongoni mwenu wakikubaliana hapa duniani kuhusu jambo lolote la kuomba, Baba yangu wa mbinguni atawafanyia jambo hilo. Kwa maana popote pale wanapokusanyika wawili au watatu kwa jina langu, mimi nipo hapo kati yao.” - KUSHIRIKISHANA MAHITAJI and CHAKULA
MATENDO 2:44 Waumini wote waliendelea kuwa kitu kimoja na mali zao waligawiana.
(A) MAHITAJI:
- Kanisa la kwanza walitilia mkazo jambo hili – MATENDO 2:45 “…waliwagawia watu wote vitu kulingana na uhitaji wa mtu”.
- Wote kwa pamoja walisaidia mahitaji ya – wajane na masikini
- Tunamuona hata mtume Paulo akiwatia moyo kanisa la Filipi kuendeleza utaratibu huu na jinsi ya kufanya – WAFILIPI 2:4 “… kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali mambo ya wengine”.
- Hivyo utaratibu huu ni vyema ukaendelezwa makanisani mwetu leo na kuzidi kufanya kwa kadri ya uwezo wetu kutatua SHIDA HALALI zilizoko kati yetu
MATENDO 2:45 Walikuwa wakiuza mali na vitu vyao kisha wakagawana fedha kadiri ya mahitaji ya kila mmoja, WAFILIPI 2:4 Pasiwe na mtu anayetafuta faida yake mwenyewe tu bali faida ya mwenzake.
(B): CHAKULA:
Waumini yatupasa kuelewa kuwa ndani ya ushirika tunahitaji kushirikiana na kuonyesha upendo wetu katika nyakati zote – MATENDO 2:44 – “Na wote walioamini walikuwa mahali pamoja, na kuwa na vitu vyote shirika” MATHAYO 9: 9-10 Yesu aliondoka hapo, na alipokuwa anakwenda zake, alimwona mtu mmoja aitwaye Mathayo, ameketi katika ofisi ya ushuru. Basi, Yesu akamwambia, “Nifuate.” Naye Mathayo akainuka, akamfuata.
10 Yesu alipokuwa nyumbani ameketi kula chakula, watozaushuru wengi na wahalifu walikuja wakaketi pamoja naye na wanafunzi wake.
HITIMISHO:
MATENDO 2:47 wakimsifu Mungu na kuwapendeza watu wote. Kila siku Bwana akaliongeza kanisa wale waliokuwa wakiokolewa.