JUMAMOSI 28 JANUARI 2023
SHUKRANI NA MAHITAJI BINAFSI
1. Mshukururu Mungu atendaye mambo makubwa kwa wale wamwitao kwa roho ya unyenyekevu Luka 17:11-19; Waefeso 3:20 – 21; Zaburi 107:1 – 9
• Mshukuru Mungu kwa uzima, afya njema, ulinzi, mafanikio.
• Mshukuru Mungu kwa neema ya wokovu Efeso 2:8 – 9
• Mshukuru Mungu kwa familia aliyokupa, na kwamba amewalinda na kuwatunza – wazazi, mwenza, Watoto, ndugu.
• Mshukuru Mungu kwa kuwa mpaji wako Zaburi 132:15
2. Ombea mahitaji yako binafsi, familia yako kadri Roho Mtakatifu atakavyokuongoza Isaya 1:18 Wafilipi 4:6; 1 Yohana 5:14 – 15
• Ombea mahitaji ya kiroho – Omba Mungu akusaidie kukua kiroho, uaminifu kwa Mungu, kwa kanisa na katika kumtumikia.
• Ombea mahitaji yako ya kimwili – Omba Mungu akupe uzima, afya njema, ulinzi, mafanikio
• Omba Mungu afanikishe malengo na mipango yako