MAHITAJI MATATU MUHIMU KWA KILA MKRISTO
- Mkristo ni mtu yeyote anaemwamini Kristo kama Bwana na Mwokozi wa maisha yake
- Mahitaji / Hitaji ni jambo lolote lenye umuhimu / ulazima mkubwa katika maisha ya mtu
- Yaani – mtu akipata jambo hilo maisha yake yanaweza kuendelea mbele / vyema
- Ikiwa tunasema chakula, malazi, na mavazi ni mahitaj ya msingi kwa mtu yeyote; basi
- Kulingana na mtume Paulo – Neema ya Bwana Yesu Krsto, Pendo la Mungu, na Ushirika wa Roho Mtakatifu ni mahitaji ya muhimu sana kwa mkristo- 2 WAKORINTHO 13:14
- Mtume Paulo alionyesha umuhimu wa mambo yaha 3 katika maisha ya wakristo kwa kuyafanya kama salamu yake ya mwisho au neno la kuwaaga wakristo na makanisa yote aliyoyaandikia nyaraka – mfano: 2 WATHESALONIKE 3:17-18
- Ikumbukwe kuwa maneno ya mwisho mtu anayopewa yanamaana kubwa sana na yapasa kueshimiwa – mfano wosia wa mzazi anapofika mwisho wa maisha yake
- Hii ni kusema huu ndio wosia wa mtume Paulo kwa kanisa la kwanza na kanisa la leo
HITAJI #1. NEEMA YA BWANA YESU KRISTO
- Paulo alijua umuhimu wa Neema hii – ndiposa hakuacha kuwatakia Neema kanisa
- Ikumbukwe kuwa tumeokolewa na kupata wokovu kupitia Neema hii – WAEFESO 2:8-9
- Paulo anawaombea Neema Kanisa kwani alijua Neema itazidi kuwafanyia wokovu, kuwafundisha kukataa uovu, kuwawezesha kutenda mema, na pia waweze kuishi maisha ya haki na utauwa duniani – TITO 2:11-12 (The Same to us today)
HITAJI #2. PENDO LA MUNGU BABA
- Paulo haishii kuona Neema tu bali pia analiona Pendo la Mungu kwani ndilo kiini cha sisi kupokea Neema ya Kristo na kupata uzima wa milele – YOHANA 3:16
- Pendo la Mungu zaidi ya kutupa uzima wa milele, pia linatupatanisha na Mungu Baba na kufutilia mbali dhambi zetu – 1 YOHANA 4:9-10
HITAJI #3. USHIRIKA WA ROHO MTAKATIFU
- Paulo alijua umuhimu wa mkristo kuwa na ushirika na Roho Mtakatifu – kwani yeye ni msaidizi wetu na hutufundisha kumjua Mungu zaidi – YOHANA 14:16, 26
- Ushirika na Roho Mtakatifu huzalisha tunda la Roho ndani yetu – WAGALATIA 5:22-23
- Hutupa kuishi maisha yenye furaha, amani, imani na tumaini kutokana na uwezesho wa nguvu za Roho Mtakatifu – WARUMI 15:13
Mwisho, maombi yangu ni kila mmoja wetu afanye jitihada ili kutopungukiwi na Neema ya Kristo, Pendo la Mungu, na Ushirika uliohai na Roho Mtakatifu katika maisha yake ya imani.
TUOMBE na kushiriki Neema:
“Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, na upendo wa Mungu Baba, na Ushirika wa Roho Mtakatifu ukae nasi sote sasa na hata milele, Amen”.







