MSHUKURU BWANA KWA MOYO WAKO WOTE. ZABURI 9:1 – 2; 103: 1 – 6
Sababu za kumshukuru Bwana: Zaburi 103: 1 – 6 Ulinzi, Ukombozi, msamaha, Wokovu, uponyaji, amani, na baraka nyingine nyingi.
- MSHUKURU BWANA KWA MOYO WAKO WOTE.
Zaburi 9:1 – 2;103:1
Zaburi 9:1a “Nitamshukuru Bwana kwa moyo wangu wote.
Maneno saba ya Kiebrania yenye njia tofauti za kumsifu Bwana:
“Barak” – kumtukuza Bwana kwa kupiga magoti, kuinama na kulala chini.
Psalm 95:6 Njoni, tuabudu, tusujudu, Tupige magoti (barak)mbele za BWANA aliyetuumba.
- “Halal/tehillah” – kumtukuza Bwana kwa mziki, kucheza na kelele za shangwe.
Zaburi 149: 3 Na walisifu (halal) jina lake kwa kucheza, Kwa sauti tamu ya matari na kinubi.
- “Yadah” – kumtukuza Bwana kwa kumuinulia mikono.
Zaburi 63:4 Ndivyo nitakavyokubariki maadamu ni hai;Kwa jina lako nitaiinua mikono yangu (Yadah).
- “Shabach” – kumtukuza Bwana kwa kelele za shangwe na makofi ya furaha.
Zaburi 47:1 “Enyi watu wote, pigeni makofi, Mpigieni Mungu kelele kwa Sauti ya shangwe (habach).
- Zamar – kumtukuza Bwana kwa kupiga vyombo vya mziki kwa ustadi.
Zaburi 33:2 Mshukuruni BWANA kwa kinubi, Kwa kinanda (zamar) cha nyuzi kumi mwimbieni sifa.
- Towdah – ibada ya shukrani inayoambatana na sadaka, matoleo mabalimbali na kuondoa nadhihri au ahadi.
Zaburi 50: 14 Mtolee Mungu dhabihu za kushukuru (towdah); Mtimizie Aliye Juu nadhiri zako.
2. SHUKRANI INAHUZISHA KUSHUHUDIA MATENDO YA BWANA.
Zaburi 9:1b; Zaburi 66:5; 1 Mambo ya Nyakati 16:8
Zaburi 9:1b “Nitayasimulia matendo yako yote ya ajabu;
3. SHUKRANI HUHUSISHA KUTOA.
Zaburi 50:14 -15; Zaburi 116:12 – 14; Kumbukumbu la Torati 16:16 – 17
Aya kuu…Kumbukumbu la Torati 16:16-17
“…. Mtu ye yote asiende mbele za BWANA mikono mitupu: 17 Kila mmoja wenu lazima alete zawadi kwa kadiri ya jinsi ambavyo Yehova Mungu wenu amewabariki.