MTAKENI MUNGU NA NGUVU ZAKE

MTAKENI MUNGU NA NGUVU ZAKE

1 MAMBO YA NYAKATI 16:11–18

Andiko hili ni sehemu ya wimbo wa shukrani wa Daudi kwa Bwana. Daudi aliutoa baada ya Sanduku la Mungu kuletwa na kuwekwa katika hema alilokuwa ameliandaa huko Yerusalemu. Sanduku hilo lilikuwa limekaa nyumbani kwa Obed-edom kwa muda wa miezi mitatu na kuleta baraka nyingi.

Kumtaka Mungu na nguvu zake ni ile ya halikumhitaji / kumtafuta kwa bidii siku zote na wakati wote. Daudi alifanya juhudi kubwa kuleta na kurejesha Sanduku la Bwana kule Yerusalemu kwa sababu alifahamu thamani yake. Sanduku liliwakilisha uwepo wa Mungu na baraka zinazotokana nalo.

Katika maisha, watu / makampuni hutumia muda, nguvu na mali nyingi kutafuta vitu wanavyoamini vina thamani. Mfano mzuri ni uwekezaji mkubwa unaofanyika katika sekta ya madini. Watu wako tayari kuwekeza sana kwa sababu wanatarajia kupata kitu chenye thamani na faida kubwa zaidi.

Vivyo hivyo, kumtaka au kumtafuta Mungu na nguvu zake ni jambo la muhimu sana kwa kila mwamini. Hatupaswi kumtaka Mungu kwa sababu ya mahitaji na changamoto za maisha tulizonazo tu, bali zaidi kwa ajili ya uzima wa milele na maisha matukufu yajayo mbinguni.

1. TUMTAKE MUNGU NA NGUVU ZAKE SIKU ZOTE

* Kumtaka Mungu hutuvuta kwake na kutufanyakudumu katika uwepo wake.

* Ni ishara ya kutambua mamlaka na ukuu wa Mungu pamoja na kukiri kwamba tunamhitaji.

* Tunamtaka na kunamtafuta Mungu kwa sababu anapatikana — Mithali 8:17.

* Mungu mwenyewe anawatafuta wale wanaomtafuta — Zaburi 14:2.

* Tunamtafuta kwa imani, tukiamini kwamba yupo na huwapa thawabu wale wanaomtafuta — Waebrania 11:6.

* Tunapokuwa na Mungu na nguvu zake, tunakuwa na yote tunayohitaji.

2. TUMTAKE MUNGU NA NGUVU ZAKE KWA SABABU YEYE NI MWEMA

Tafakari maneno haya: “Mungu ni mwema kila wakati, na kila wakati Mungu ni mwema.”

* Wema wa Mungu unaonekana kupitia yale anayotutendea.

* Maajabu na miujiza yake hutukumbusha wema wake — Vs. 12.

* Tunamtata kwa sababu yeye ndiye Mungu wa maisha yetu yote —Vs. 14.

* Kumtafuta Mungu hutuwezesha kuonja na kuona  wema wake – Zaburi 34:8.

3. TUMTAKE MUNGU NA NGUVU ZAKE KWA SABABU YA AGANO LAKE

* Mungu alifanya agano la kudumu na Abrahamu — Mwanzo 22:18.

* Kupitia agano hilo, tumekuwa warithi wa baraka zake, ulinzi wake, na mahitaji tunayopokea kutoka kwake — Wagalatia 3:7–8.

* Kupitia kumwamini Kristo Yesu, agano hilo limefungua njia ya wokovu wetu — Wagalatia 3:14,16.

* Agano linatufundisha kumtumaini Mungu na kuishi kwa imani katika yeye.

* Pia linatukumbusha uaminifu wa Mungu na kututia moyo kuendelea kumtaka na kumtafuta yeye Mungu.

Hitimisho:

– Tunapaswa kumtaka Mungu kwanza kwa sababu ya uungu wake, si kwa sababu tu ya nguvu zake, uwezo wake au miujiza anayoweza kutenda.

– Tumtake na kumtafuta Mungu siku zote, kwa sababu yeye yeye ni mwema, na mwaminifukwetu, na kwa sababu ya agano lake ambalo limetuwezesha kupokea wokovu kwa imani.

Join the Discussion

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top

Share with