MUNGU AMEKUWEZESHA ILI KUTUMIKA

MUNGU AMEKUWEZESHA ILI KUTUMIKA

Neno 1 Pet 4:10

UTANGULIZI

  • Petro aliwaandikia wakristo (ambao sio wayahudi) wa utawanyiko (exiled) katika mikoa 5 ya Kirumi ambayo kwa leo ni Uturuki. Aliandika kwa dhumuni la kuwakumbusha kuhusu tumaini lao, kuvumilia, utambulisho wao mpya, na  mwenendo wa heshima.
  • Katika mlango wanne ameongelea kumuishia Mungu (1 Pet 4:1-11) na mateso kwa kuwa Mkristo (1Pet 4:12-19)

SOMO 1: MUNGU NDIYE MTOA KARAMA

Karama ni nini?

  • Karama ni uwezo wa kiungu unaotolewa bure na Roho Mtakatifu kwa mwamini.
  • Karama ni zawadi ya kiroho, uwezo wa pekee, au neema inayotolewa na Mungu kwa mtu kwa ajili ya kuwatumikia na kuwajenga wengine, hasa ndani ya kanisa au jamii.
  • Mungu ndiye aliyetuumba, hivyo Yeye ndiye anayejua ni uwezo, karama gani aliokupa au unayohitaji au atakayokupa.

Utajuaje kama Mungu amekupa karama?- Roho Mtakatifu ndiye atakusaidia kutambua hilo

1 Kor 2:12, Yn 16:13-14

1 Kor 2:12

Lakini sisi hatukuipokea roho ya dunia, bali Roho atokaye kwa Mungu, makusudi tupate kuyajua tuliyokirimiwa na Mungu.

1 Kor 12:4-11
“4 Basi pana tofauti za karama; bali Roho ni yeye yule.  5 Tena pana tofauti za huduma, na Bwana ni yeye yule. 6 Kisha pana tofauti za kutenda kazi, bali Mungu ni yeye yule azitendaye kazi zote katika wote. 7 Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa kufaidiana. 8  Maana mtu mmoja kwa Roho apewa neno la hekima; na mwingine neno la maarifa, apendavyo Roho yeye yule; 9 mwingine imani katika Roho yeye yule; na mwingine karama za kuponya katika Roho yule mmoja; 10 na mwingine matendo ya miujiza; na mwingine unabii; na mwingine kupambanua roho; mwingine aina za lugha; na mwingine tafsiri za lugha;11 lakini kazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja, yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye.”

SOMO 2: KARAMA NI KWAAJILI YA HUDUMA

  • Dhumuni la kuumbwa na kupatinishwa kwetu na Mungu sio ili tuishi halafu tufe. Mungu tayari alipanga tokea awali kuwa tutende matendo mema.

Efe 2:10, (Tito 2:14)

Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo.

  • Biblia imetupa mwongozo wa nini cha kufanya na karama tulizopokea- kuhudumiana.

1 Pet 4:10 

“kila mmoja kwa kadiri alivyoipokea karama, itumieni kwa kuhudumiana; kama mawakili wema wa neema mbalimbali za Mungu.”

1 Kor 14:12 “Vivyo hivyo na ninyi, kwa kuwa mnatamani sana kuwa watu wenye karama za roho, takeni kwamba mzidi sana kuwa nazo ili kulijenga kanisa.”

  • Mtu akikupa zawadi huwa anakupa kitu ambacho utatumia, kitachokusaidia/kukuhudumia. Vivyo hivyo Mungu ametupa karama ili tuhudumiane.

1 Kor 12:7-10
“7 Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa kufaidiana. 8  Maana mtu mmoja kwa Roho apewa neno la hekima; na mwingine neno la maarifa, apendavyo Roho yeye yule; 9 mwingine imani katika Roho yeye yule; na mwingine karama za kuponya katika Roho yule mmoja; 10 na mwingine matendo ya miujiza; na mwingine unabii; na mwingine kupambanua roho; mwingine aina za lugha; na mwingine tafsiri za lugha;

  • Mbinguni hamna uhitaji wa neno la hekima, maarifa, uponyaji etc(1 Kor 12:8-10)  kwahiyo karama hizi ni za kutumia hapa duniani.

Rum 12:4-8 SUV
“4 Kwa kuwa kama vile katika mwili mmoja tuna viungo vingi, wala viungo vyote havitendi kazi moja; 5 Vivyo hivyo na sisi tulio wengi tu mwili mmoja katika Kristo, na viungo, kila mmoja kwa mwenzake. 6 Basi kwa kuwa tuna karama zilizo mbalimbali, kwa Kadiri ya neema mliyopewa; ikiwa unabii, tutoe unabii kwa Kadiri ya imani; 7 ikiwa huduma, tuwemo katika huduma yetu; mwenye kufundisha, katika kufundisha kwake; 8 mwenye kuonya, katika kuonya kwake; mwenye kukirimu, kwa moyo mweupe; mwenye kusimamia kwa bidii mwenye kurehemu, kwa furaha.”

  • Mungu hakumbariki Abramu ili awe na baraka ila alimalizia kwa kumwambia ili awe baraka kwa wengine.

Mwa 12:1-2 BWANA akamwambia Abramu, Toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonyesha; nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka.

SOMO 3: KUTUMIKA NI UWAKILI MWEMA WA NEEMA YA MUNGU

1 Pet 4:10, Luka 12:42

“Bwana akasema, Ni nani, basi, aliye wakili mwaminifu, mwenye busara, ambaye bwana wake atamweka juu ya utumishi wake wote, awape watu posho kwa wakati wake?”

  • Mungu amekupa neema yake ili uitumie. Unaitumiaje?- ni kwa kutumika.
  • Kutokutumika ni kupokea neema ya Mungu bure.

1 Kor 15:10

“Lakini kwa neema ya Mungu nimekuwa hivi nilivyo; na neema yake iliyo kwangu ilikuwa si bure, bali nalizidi sana kufanya kazi kupita wao wote; wala si mimi, bali ni neema ya Mungu pamoja nami”

2 Kor 6:1

“Nasi tukitenda kazi pamoja naye twawasihi msiipokee neema ya Mungu bure”

  • Yesu pia alikuja kutumika (Marko 10:45 SUV “Kwa maana Mwana wa Adamu naye hakuja kutumikiwa, bali kutumika, na kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi)
  • Tukiongelea swala la uwakili huwa tunarudi kwenye mfano ulioandikwa katika Mat 25: 14-30
  • Aliepewa talanta 5 na 2 waliambiwa (Mat 25:21&23 BHN) “Vema, mtumishi mwema na mwaminifu. Umekuwa mwaminifu katika mambo madogo, nitakukabidhi makubwa”
  • Aliepewa talanta 1 aliambiwa (Mat 25:26,28,30 BHN)“ 26 Wewe ni mtumishi mwovu na mvivu! …… 28 Basi, mnyanganyeni hiyo fedha mkampe yule mwenye talanta kumi…….  30 Na kuhusu huyu mtumishi asiye na faida, mtupeni nje gizani!”
  • Efe 2:10 inasema Mungu alituumba ndani ya Kristo Yesu ili tufanye matendo mema.

HITIMISHO

1 Pet 4:1-6

×Note: To download, click the button. If it doesn't work, right click, then click "Save Link As." Download only works if media is stored within this site. Download Video

Join the Discussion

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top

Share with