TWENDE KWA YESU

MATHAYO 11:28-30

  • Yesu aliposema twende kwake ili atupumzishe na mizigo, ni wazi kwamba alijua watu wengi wamebeba mizigo mizito tena inayowalemea
  • Mizigo hii ya shida na mateso imewafanya watu wengi hata kukata tamaa na kuvunjika moyo katika maisha yao
  • Yesu Kristo kwa kuzijua shida na mateso watu wanayopitia anatoa wito uliojaa faraja na huruma kwamba tunapolemewa, basi tukimbilie kwake
  • Huu ni wito uliojaa pumuziko na tumain la kweli katika imani zetu kwake 

I#      YESU ATATUPATIA PUMZIKO             – Mathayo 11: 28-30

  • Ikumbukwe kuwa kwa Yesu kunapatikana pumziko la kweli – lenye raha
  • Mara nyingi mtu aliyechoshwa na kulemewa na mizigo huitaji pumziko 
  • Pumziko linampa mtu nguvu na hali mpya ya kuendelea mbele tena
  • Pumziko laweza kumpa mtu mawazo na mbinu mpya ili kuendelea mbele
  • Yesu ameahidi kutupa pumziko wale wote tuliolemewa na mizigo mingi
  • Hii yaweza kuwa mizigo ya njaa, magonjwa, umaskini, vita na mapigano (kimwili, kiroho, familia/ukoo, mahusiano, na hata katika utumishi)
  • Ili Yesu atupumzishe na hayo yote, lazima tuchukua hatua ya kumwendea 
  • Tumwamini, tumtegemee, tumuombe kama yeye mwenyewe alivyofanya mbele za Baba yake – Luka 6:12, nasi tuendelee kuomba – Mathayo 7:7-8

II#     YESU ATATUONGEZEA IMANI            – Luka 17:1-5

MWISHO, Mathayo 8:23-27 – kumwendea Yesu tunapolemewa na mizigo ni hatua ambayo hata wanafunzi wa Yesu mwenyewe waliichukua. Hivyo, twendeni kwa Yesu ili atupumzishe na mizigo ya dunia hii na kutuongezea imani. 

Join the Discussion

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top