SIKU 21 ZA KUFUNGA NA KUOMBA JUMAMOSI 11 JAN 2025 KUMWABUDU MUNGU KATIKA ROHO NA KWELI. 

KUMWABUDU MUNGU KATIKA ROHO NA KWELI. 

1.Jiombee ili uweze kuishi maisha ya kumwabudu Mungu katika nyakati zote (wakati wa mafanikio na majaribu pia). Omba moyo wa ibada kila siku. Yohana 4:23-24,  Zaburi 95:1-2

2. Ombea Kanisa lako la mahali na makanisa yote ya PAG na katika mwili wa Kristo, kuwa na ibada zenye nguvu za Roho Mtakatifu na uwepo mwingi wa Mungu ili watu wasimwabudu Mungu kwa mazoea. Ombea ujazo wa Roho Mtakatifu kwako na kwa washirika wenzako wa kanisa la mahali.  Zaburi 27:4

3. Ombea Wachungaji na viongozi wa PAG Tanzania  pamoja na Mwili wa Kristo kuhudumu kwa uwezo na udhihirisho wa nguvu za Roho Mtakatifu na ishara na miujiza vionekane.         1 Wakorintho 2:1-5, Matendo 5:15

4. Omba Mungu ainue vipawa vya muziki na utunzi wa nyimbo kwa waimbaji BINAFSIvikundi vya KWAYA na vya KUSIFU na KUABUDU katika kanisa la mahali na katika mwili wa Kristo Tanzania. Zaburi 33:1-4, 1 Nyakati 25:6-7

Join the Discussion

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top