SIKU 21 ZA KUFUNGA NA KUOMBA 13 JANUARI 2025
KUJAZWA NGUVU ZA MUNGU KWA AJILI YA KAZI YA UINJILISTI, KUPANDA MAKANISA NA UMISHENI. Mathayo 28:18-20
1. Omba ujazo wa nguvu za Roho Mtakatifu kwa ajili ya kazi ya Mungu. Matendo 1:4-5, 8
– Omba nguvu za Mungu za kuitenda kazi ya Mungu kama mtu binafsi. Matendo 1:8
– Omba kwa ajili ya uwezesho wa vipawa vya kutenda kazi yake. 1 Wakorintho 12:4-6
– Mwombe Mungu akuoneshe kipawa chako kupitia Roho Mtakatifu Warumi 12:3-8
2. Ombea Idara ya Uinjilisti na Umisheni katika ngazi zote PAG Tanzania Kuanzia kanisa la mahali hadi Taifa.
– Ombea Viongozi ili Mungu awatumie na kuwapa mikakati ya kuongeza kasi ya uinjilisti, umisheni na upandaji wa makanisa mapya. Warumi 10:9-17
– Ombea Bwana alete watenda kazi shambani mwa Bwana. Luka 10:2
– Ombea viongozi na makanisa yote ya PAG Tanzania ili wawe na mtazamo wa uinjilisti na umisheni. 1 Wakorintho 9:16
– Ombea washirika wawe na moyo wa kuwafikia wengine na injili ya Kristo.
3. Ombea upandaji wa makanisa mapya katika mikoa, wilaya, tarafa, kata, vijiji na hata vitongoji ambavyo PAG Tanzania haina makanisa. Warumi 15:20
– Ombea upandaji wa makanisa katika ukanda wa Pwani ya Tanzania (maeneo yaliyotawaliwa na Uislamu), Zanzibar na watu jamii nyingine ambazo hazijafikiwa na Injili kwa kupanda makanisa zaidi katika maeneo hayo.
– Upatikanaji wa Viwanja, Watu, Fedha n.k
4. Ombea kazi ya Umisheni wa nje ya Tanzania. Omba Mungu ainue watu wenye sifa na uwezo wa kupanda makanisa katika mataifa mbalimbali ya Afrika (na hata nje ya Afrika) kama vile Rwanda, DR Congo, Comoros, Madagascar, Sudani na Msumbiji, n.k
– Ombea vyuo vyetu vizalishe watu wenye uwezo wa kufanya umisheni. Elimu ya kuweza kufanya huduma nje ya mazingira tuliyozoea, Lugha, Tamaduni n.k
– Ombea waalimu wote wa shule na vyuo vyetu vyote vya biblia ili waandae watumishi wa kanisa kwa ubora wa hali ya juu.
– Ombea washirika wote wa PAG Tanzania wawe na mzigo na mtazamo wa kimisheni ili wajitoe kwa hali na mali zao kuisapoti kazi ya umisheni kwa viwango vya juu Zaidi.