SIKU 21 ZA KUFUNGA NA KUOMBA JUMATANO 15 JANUARI 2025 – KUOMBA KWA AJILI YA MAHUSIANO (UCHUMBA), NDOA NA FAMILIA

SIKU 21 ZA KUFUNGA NA KUOMBA JUMATANO 15 JANUARI 2025
KUOMBA KWA AJILI YA MAHUSIANO (UCHUMBA), NDOA NA FAMILIA
Waefeso 5:25-33, 2 Wakorintho 6:14-18, Malaki 2:14-16, 1 Samuel 1:1-20, 1 Timotheo 3:1-9, 1 Timotheo 5:3-8

1.⁠ ⁠Ombea viongozi wa PAG Tanzania katika ngazi mbalimbali ili waweze kuandaa na kufundisha masomo yenye misingi ya kibiblia na yanayoleta mabadiliko chanya katika uchumba, ndoa na familia.
•⁠ ⁠Ombea wakurugenzi wa idara ya wanawake na wanaume kuanzia ngazi ya taifa mpaka kanisa la mahali Mungu
awatumie kutoa semina na mafundisho ya uchumba, ndoa na familia ili tuwe na ndoa zenye afya na ustawi.

2.⁠ ⁠Ombea vijana ambao wanahitaji kuoa au kuolewa ili Mungu awaongoze kupata wenzi sahihi wenye hofu ya Mungu

3.⁠ ⁠Ombea wana ndoa wote katika makanisa yetu (na makanisa mengine pia) ili waishi maisha ya furaha na amani na yanayompendeza Mungu.
•⁠ ⁠Omba kinyume na roho za mafarakano na migawanyiko katika ndoa na familia.
•⁠ ⁠Ombea ndoa za watumishi wa Mungu wachungaji/maaskofu/waalimu na viongozi wa ngazi
zote ziwe na ustawi na za mfano kwa kanisa na kwa jamii.
•⁠ ⁠Ombea baraka za Watoto kwa ambao wanamngoja Bwana ili Mungu awajalie kupata watoto
wa kiume na kike.

4.⁠ ⁠Ombea wajane, wagane, yatima na wazazi wasiokuwa na wenzi wao (single parents)
•⁠ ⁠Mungu awasaidie kuishi maisha yenye furaha na amani na yanayompendeza.
•⁠ ⁠Omba kwa ajili ya mahitaji yao kwamba Mungu akawapiganie.

Join the Discussion

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top