SIKU 21 ZA MAOMBI NA KUFUNGA JUMAMOSI  TAREHE 18 JAN 2025KUOMBEA USHIRIKA – WENZA NA USHIRIKIANO.

KUOMBEA USHIRIKA – WENZA NA USHIRIKIANO.
         Kipindi cha Kwanza maombi binafsi 
1. Ombea mahitaji binafsi, Mungu abariki kazi za Mikono yako. Kumbukumbu la torati 28:1-12 

– Mungu akuunganishe na watu sahihi kwenye kazi zako, mashamba au chanzo chochote cha kipato chako mwaka huu.

– Mungu akupe kibari chake ,akili nzuri na nguvu za kufanya kazi na  kupata utajiri. (Kumbukumbu la torati 8:18, Mithali 3:4-6)

2. Ombea mipango yote ya kiuchumi uliyonayo mwaka huu yakafanikiwe. Mithali 16:1

3. Ombea mahitaji yako mengine:- Afya, ulinzi, Watoto, ndoa, na kila jambo jema unalo litaka mwaka huu. Zaburi 34:9-10.

Kipindi cha Pili maombi ya kanisa.

4. Ombea Mungu aliunganishe na kuendeleza mahusiano kati ya kanisa letu la PAGT, DPC na mashirika mengine ulimwenguni yenye maono na utume unaofanana kiimani na kimkakati ili kutimiza kusudi kuu. 2 Wakorintho 6:14-17.

– Ombea ushirika wenza kati ya kanisa la PAGT, DPC na Pentecostal Assemblies of God of Canada (PAOC), na PAG na huduma Compassion International Tanzania wanao husika na huduma ya mtoto na vijana. Muhubiri 4:12, Amosi 3:3

5. Ombea ushirikiano katika huduma mbalimbali ya kanisa la PAGT na Council of the Pentecostal Churches in Tanzania (CPCT) ili kulitimiza kusudi la Mungu hapa Tanzania. 
1 Wakorintho 3:6-11, Mithali 27:17 

Join the Discussion

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top