SIKU 21 ZA MAOMBI NA KUFUNGA: JUMATATU 20 JANUARI 2025 – KUOMBEA MAENDELEO YA WASHIRIKA, KANISA LA MAHALI, PAG (T) NA MWILI WA KRISTO

SIKU 21 ZA MAOMBI NA KUFUNGA: JUMATATU 20 JANUARI 2025
KUOMBEA MAENDELEO YA WASHIRIKA, KANISA LA MAHALI, PAG (T) NA MWILI WA KRISTO.

  1. Ombea upenyo wa kiuchumi wa washirika wote wa makanisa ya PAG Tanzania, na mwili wa Kristo. 2 Wathesalonike 3:10-12, Mithali 10:22, Isaya 43:19 
    – Omba Mungu abariki kazi za mikono yetu. 
    – Ombea upenyo kwa wafanyabiashara, wakulima na wafanyakazi wote ili wabarikiwe mwaka huu wa 2025.
  2. Ombea maendeleo ya kanisa lako la mahali. Omba Mungu apanue mipaka ya kanisa lako lizidi kulitumikia kusudi la Mungu hapa duniani. Luka 6:38, Malaki 3:10-13 
    – Omba Mungu awabariki wachungaji, watumishi wengine kiuchumi 
    – Ombea moyo wa utoaji kwa washirika wamtolee Mungu zaka na matoleo mengine ili kufanikisha malengo ya kanisa katika ngazi zote.
  3. Ombea viongozi wa PAG Tanzania kuanzia ngazi ya taifa mpaka kanisa la mahali ili wawe na umoja katika kuutekeleza Mpango Mkakati wa PAG Tanzania wa miaka kumi 
    (2021-2031)
    . Zaburi 133, Waefeso 3:20  
    – Ombea Kamati Tendaji (Askofu Mkuu, Makamu Askofu Mkuu, Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu) na Halmashauri Kuu ili Mungu awajalie hekima katika kupanga na kusimamia maendeleo ya Kanisa letu la PAG Tanzania kwa utukufu wa Mungu
    – Ombea Moyo wa Umoja na ushirikiano katika kila idara ili kujenga kanisa la PAG Tanzania
    – Ombea wachungaji na makanisa wamtolee Mungu zaka na michango mingine kwa moyo na kwa uaminifu ili kufanikisha malengo ya PAG Tanzania katika ngazi zote.

Join the Discussion

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top