SIKU 21 ZA KUFUNGA NA KUOMBA: IJUMAA 24 JANUARI 2025

Maombi ya Mfungo Siku ya 19,  Ijumaa 24 Januari 2025

MWABUDU MUNGU NA KULIINUA JINA LAKE 

  1. Mwabudu na kumwadhimisha Mungu kwa uaminifu wake na Kwa Ukuu wake. 
    Mtukuze Mungu kwa kuwa fadhili zake zadumu hata milele. Fadhili zake kwenye Afya, Familia,…
    – Mtukuze Mungu kwa kukuwezesha kuomba tangu siku ya kwanza hadi leo.
    – Mtukuze Mungu kwa Neema yake na kukuwezesha katika yote unayoyafanya katika maisha yako Mf ; Kazi, Biashara, Shule, Chuo, Safari zako mbali mbali …
  2. Zaburi 34:3, Zaburi 103:21-22, Luka 1:46, Warumi 11:36

2. Msifu kwa kutaja majina yake kama vile;

  • El-Shadai (Mungu anayejitosheleza, Mwenye nguvu..)

  • Yehova-Yire (Mungu mpaji wetu), Genesis 22:14 

  • Yehova-Rapha (Mungu atuponyaye), Kutoka 15:26

  • Yehova-Shama (Mungu yuko hapa), Ezekiel 48:35, Isaiah 49:15 

  • Yehova Nissi (Bwana Ushindi wetu) 
Yehova-Shalom (Mungu ni amani yetu). Ufunuo 4:11, 2 Samweli 22:4, Zaburi 48:13.

3. Mwombe Roho Mtakatifu akusaidie kuomba katika Roho. Yuda 1;20

Join the Discussion

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top