Mwongozo wa maombi ya wiki kwa idara ya Vijana DPC
1. SHUKRANI
~ Mshukuru Mungu kwa upendo wake kwetu Zaburi 92:1-2
~ Mshukuru Mungu kwa upaji na ulinzi wake katika maisha yetu Zaburi 23:1-6
~ Mshukuru Mungu kwa uongozi wa kanisa kutupa wiki ya kutumika
2. MAOMBI YA TOBA
~ Omba Mungu atusamehe dhambi zetu Luka 15:18-20
~ Omba Mungu atusamehe kwa kutokutumika katika ufalme wake kulingana na karama alizotupa Luka 6:46,
1Petro 4:10
~ Mwombe Mungu atusamehe kwa kutokutumia karama / fursa alizotupa Wagalatia 5:13-14
3. MAHUDHURIO
~ Omba vijana tuwe na shauku ya kuhudhuria wiki nzima ya vijana, Zabri 122:1
~Simama kinyume na vizuizi ambavyo vinaweza kuwazuia vijana kuhudhuria ratiba ndani ya wiki ya vijana. Isaya 57:14
4. OMBEA WANENAJI
~Ombea wanenaji wanene kwa ujasiri na mamlaka kutoka kwa Mungu matendo 4:18-20
~ Omba Roho Mtakatifu aseme na kila kijana kwa kutoa maelekezo maalumu kupitia wanenaji Yohana 14:26
~ Omba udhihirisho wa Roho Mtakatifu katika vipindi vyote wakati wa wiki ya Vijana

