KUTEMBEA HATUA KWA HATUA NA ROHO MTAKATIFU. Wagalatia 5:25.
Wagalatia 5:25 ni Mstari wetu wa kusimamia – Mstari Mkuu au Mada au Dhamira ya Week Hii Ya Vijana.
Wengi husema kwamba Roho Mtakatifu hahitaji utambulisho kwa sababu, katika imani ya Kikristo, Yeye yupo daima, ana nguvu, na anajulikana kwa karibu na wale wanaotembea katika imani. Mara nyingi huelezwa kama pumzi ya Mungu mwenyewe, Roho Mtakatifu hatambulishwi tu bali anathibitishwa Kimatendo — akituongoza, akitufariji, akituonya, na kutupa uwezo wa kiroho.
Hata hivyo, kwa ajili ya kuelewa, Tunajifunza kuhusu Roho Mtakatifu kupitia Maandiko au ushuhuda wa kibinafsi — si kumtambulisha kana kwamba ni mgeni, bali kuwasaidia wengine watambue uwepo wake na kazi yake.
Hebu Tuutafakari Mstari Mkuu.
Tukiishi kwa Roho, na tuenende kwa Roho…
- Tukiishi kwa Roho…”
→ Ikiwa maisha yetu ya kiroho yamefanywa hai katika Kristo kupitia kazi ya Roho), basi… - “…na tuenende kwa Roho.”
→ …basi mwenendo wetu wa kila siku, maamuzi, tabia, na mitazamo inapaswa kuongozwa kikamilifu na Roho huyo huyo — si tamaa za mwili, si mazoea ya dunia, bali mwelekeo wa kiroho.
Ni Jinsi Gani tunaweza kufanya Maisha yetu Yawe na uhalisia wa Uwepo wa Roho Mtakatifu (Yaani kutembea na Roho Mtakatifu ?
- Turudi Nyuma na tuitazame Ahadi ya Roho Mtakatifu.
Kwa kuona umuhimu wa Nguvu hii ya Uwepo wa Roho Mtakatifu, Tazama Maneno yesu aliyoyasema. (Umuhimu wa Kutembea na Roho Mtakatifu unaonekana kwa namna nyingi kweny maandiko lakini – Uzito Zaidi uko katika maneno aliyoyasema yesu mwwnyewe.
Yohana 16:7 – Lakini mimi nawaambia kweli; Yawafaa ninyi mimi niondoke; kwa maana nisipoondoka, huyo Msaidizi hatakuja kwenu; lakini mimi nikienda, nitampeleka kwenu.
Na pia Yesu Aliona Hamna Jisni tunayoweza kuzishinda Nguvu za ulimwengu huu, bila kuwa na Nguvu za Mungu Ndani yetu haya Tunayaona Katika – Matendo ya Mitume 1:8
Lakini mtapokea nguvu, Roho Mtakatifu akiwajilia juu yenu, nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na Yudea yote, na Samaria, na miisho ya dunia.
Nguvu, Tuitazame kwa upana –Nguvu ni uwezo, au Ushawishi, wa Kuathiri au kubadilisha kitu Fulani
au uwezo wa kushinda.
Kuzaliwa Mara Ya Pili – Ni Kuzaliwa katika Roho Na hii hutokea tunapo tubu dhambi na kumpokea Yesu kua Bwana na Mwokozi wa Maisha yetu – Roho Mtakatifu ndio chanzo chetu cha kuzaliwa Mara ya Pili. 1 Wakorintho 12:3
Yohana 16:8 “Naye atakapokuja, atauhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi, na haki, na hukumu.”
Roho Mtakatifu Ndio Hutushawishi (Convict) Kuhusu, Thambi, Haki ya Mungu na Hukumu Ijayo
Tunaenendaje kwa Roho
- Lazima uwe Umezaliwa Upya -Yohana 3:5–6)
- Kua mtiifu kwa Uongozi wa Roho Mtakatifu – Kadri unavyotii, ndivyo sauti ya Roho itazidi kuwa wazi kwako. (Waefeso 4:30)
- Jilishe katika Neno la Mungu – Waefeso 6:17
- Hakikisha -Tunda la Roho linadhihirika ndani yako – Galatia 5:22–23 – Upendo, Furaha, Amani, Uvumilivu, Uaminifu, Ukarimu, Upole, Kujizuia
- Omba Mara kwa Mara -Waefeso 6:18
- Epuka Kutawaliwa na Mwili -Galatia 5:16)
- Fanya ushirika na waaminio
Inapendeza kuona kua Emphasis ya Roho Mtakatifu Imepewa kipaumbele na Uongozi wa Vijana. Kama Vile Yesu alivyoonyesha Umuhimu wa kuenenda katika Nguvu ya Roho Mtakatifu.

