BWANA YESU ASIFIWE! Tunatumaini Mungu amewaweka salama. Tunapenda kuwataarifu yafuatayo:
i. MAOMBI YA IJUMAA. Tafadhali fahamu kwamba wiki hii hakutakuwa na Ibada ya Maombi ya Ijumaa. Maombi haya yatarejea kama kawaida Ijumaa tarehe 14 Novemba 2025.
ii. IBADA ZA JUMAPILI. Ibada za Jumapili zitaendelea kama kawaida kuanzia Jumapili hii:
- Ibada ya Kiingereza: Saa 2:00 asubuhi – Saa 4:00 asubuhi.
- Ibada ya Kiswahili: Saa 4:30 asubuhi – Saa 6:30 mchana.
iii. MIKUTANO YA SELI. Mikutano ya Seli itarejea wiki ijayo kama kawaida.
Tunawashukuru kwa ushirikiano wenu na tunawatakia baraka za Bwana.
Uongozi,
Dar es Salaam Pentecostal Church (DPC)

