MWONGOZO WA MAOMBI YA MAANDALIZI YA IBADA YA KUSIFU NA KUABUDU MWEZI WA NOVEMBA 2025

1.⁠ ⁠OMBI LA TOBA. 1 Yoh 1:8–10
•⁠ ⁠Omba toba juu yako,familia yako, huduma yako, huduma zote kanisani,waumini wote wa dpc, viongozi katika idara zote. Isaya 1:18 Zaburi 103:12
•⁠ ⁠Omba toba kwa ajili ya ndungu zako, neema ya wokovu iwafikie. Matendo 16:31 Luka 15:7 Yohana 3:16
•⁠ ⁠Omba toba kwa wale waliorudi nyuma Bwana awarejeshe tena kundini. Mit 1:32-33 Luka 15:21-24
•⁠ ⁠Omba toba kwa ajili ya kanisa la Tanzania Mungu alirejeshe katika nafasi yake na kuwa majibu kwa taifa hili. Ezekieli 36:26 Yeremia 15:19
•⁠ ⁠Omba toba kwa ajili ya taifa letu na viongozi, Mungu aponye kila moyo ulioumizwa na arejeshe kile adui alichokiiba .Nyakati 7:14 Isaya 55:7

2.⁠ ⁠OMBI BINAFSI. Efe 2:8–9
•⁠ ⁠Shukuru Mungu kwa neema yake ambayo imekubeba nyakati zote na majira yote ya mwaka huu,mwambie sikustahili ila umenistahilisha. Wagalatia5-16
•⁠ ⁠⁠Omba Nguvu za Roho mtakatifu zishuke juu yako kukuwezesha kutimiza kusudi la Mungu. Warumi 8:11 Matendo 1:8
•⁠ ⁠Omba nguvu na ujasiri mkubwa wa kufanya kile Mungu alichokuitia, kataa roho ya kufanya kazi ya Mungu kwa ulegevu. 2 Timotheo 1:7 Efeso 3:16
•⁠ ⁠Mwambie Mungu ajifunue kwako kwa upya ishara na ajabu zake ziambatane pamoja na wewe,watu watakapokuona wamtukuze Mungu. Mk 16:17 Isaya 8:18
•⁠ ⁠Jiombee roho ya utulivu ili upate kumsikia Roho Mtakatifu anapokupa maelekezo ya nini cha kufanya. Warumi 8:14 1wakorintho 2:11
•⁠ ⁠Kataa maisha ya kuanguka kwenye dhambi kila wakati. Wagalati 6:8 Yakobo 1:14-15

3.⁠ ⁠IBADA NZIMA
•⁠ ⁠Ombea ibada zote tatu—Roho Mtakatifu aguse na kubadilisha maisha. Zak 4:6
•⁠ ⁠Ombea idara zote na walioalikwa—umoja na nguvu katika roho na mwili. Efe 4:3
•⁠ ⁠Omba udhihirisho wa nguvu za Mungu: ishara, ajabu na miujiza. Mat 5:12
•⁠ ⁠Omba macho ya watu kutiwa nuru waone ukuu wa Mungu kwenye changamoto zao. Efe 1:18
•⁠ ⁠Ombea kila mshiriki ajazwe nguvu za Roho Mtakatifu kwa ibada ya kweli. Efe 5:18, Yoh 4:23
•⁠ ⁠Ombea mnenaji—upako, hekima na neno la wakati. Kol 3:16, Efe 6:19
•⁠ ⁠Ombea mahudhurio na matangazo—watu wengi wahudhurie. Mat 28:19, Mat 13:44

Join the Discussion

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top