SIKU 21 ZA KUOMBA NA KUFUNGA – DPC
JUMATANO | 7 JANUARI 2026
KAULI MBIU:
Shauku ya Kuomba na Kujua Mapenzi ya Mungu kwa Mwaka 2026
1️⃣ Shauku ya Kuomba
• Omba Roho Mtakatifu akuongoze, akufundishe, na kukusaidia kuomba sawasawa na mapenzi ya Mungu kila siku.
📖 Warumi 8:26–28
• Mwombe Bwana akupe ari mpya ya kusoma, kujua, na kulielewa Neno Lake ili tuombe kulingana na makusudi Yake.
📖 2 Timotheo 3:16–17; Warumi 12:2
2️⃣ Urejesho
• Omba Mungu akurudishie maradufu yale yote yaliyopotea katika maisha yako.
📖 Yoeli 2:25–27; Zekaria 9:12
3️⃣ Kujua Mapenzi ya Mungu kwa Maisha Yako
• Ombea mapenzi ya Mungu katika mipango yako binafsi na ya familia kwa mwaka 2026.
📖 Wakolosai 1:9; Waefeso 5:17
• Omba shauku ya kusimama imara na kukaa katika kusudi la Mungu.
📖 Zaburi 27:4







