SIKU 21 ZA KUOMBA NA KUFUNGA – JUMAMOSI, 10 JANUARI 2026
🙏 OMBEA UPENYO WAKO WA KIFEDHA / KIUCHUMI 🌟
1️⃣ Ombea upenyo wako wa kiuchumi, na wa familia yako.
Mungu akufunulie fursa ya kazi, biashara, au kujiajiri iliyo mbele yako.
📖 Wafilipi 4:19, Mhubiri 11:4-6
2️⃣ Omba Mungu aimarishe uchumi wako na vyanzo vyako vya mapato.
Katika kazi yako, biashara yako, nk. 📖 Zaburi 90:16-17
3️⃣ Omba Mungu aibariki kazi ya mikono yako na kukufanikisha kila eneo. 📖 Kumbukumbu 28:5-6, Zaburi 90:17
4️⃣ Omba Mungu akupe kujibidiisha (bidi) katika majukumu yako yote.
📖 Mithali 13:4, Mithali 12:24, Filipi 4:13
5️⃣ Omba Mungu akupe moyo wa utoaji kwa ajili ya kazi yake.
📖 Kumbukumbu 8:18, Isaya 48:17
6️⃣ Kemea roho inayopingana na uchumi wako.
Ombea dhidi ya madeni sugu, magonjwa sugu, rushwa, na usumbufu mwingi kwa wanaoomba ajira.
📖 2 Wafalme 4:1-7, Kutoka 23:8, Marko 5:25-26, Mhubiri 7:7
🕊️ Jiunge nasi katika kumtafuta Mungu kwa ajili ya upenyo wetu wa kifedha na kiuchumi!

